Na Mahmoud Ahmad Arusha
Serikali inatambua ukatili
wanaokumbana nao watoto ndio maana imeandaa mkakati wa taifa wa
kukabiliana changamoto 8 zitakazo shuhulikiwa ili kutatua na kupunguza
masuala ya ukatili hapa nchini wanazokumbana wazee,watoto na kinamama
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri
wa Afya maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Dkta Hamis Kigwangala
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa huduma ya malezi na masaada wa
kisaikolojia kwa watoto uliondaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya
Repssi unaondelea jijini hapa.
Dkta Kigwangala amesema kuwa
kulikuwa na mikakati zaidi ya 8 na sasa wanakuja na mkakati mmoja
unaoanza mwaka huu hadi mwaka 2022 lengo kuu ni kupambana na ukatili
dhidi ya ustawi wa maendeleo ya motto na kutoa ushauri nasaha
utakaosaidia taifa siku za usoni kimaendeleo.
Amesema kuwa mikakati mingi
imelenga kuondoa suala zima la ukatili na mkutano huo utasaidia kuja na
njia nzuri ya kuweza kusaidia taifa letu kuondokana na ukatili wa
kijinsia ambao unashika kasi hapa nchi kwani takwimu zinaonyesha kati ya
watoto saba mmoja amefanyiwa kuatili uwe wa kingono au kufanyishwa
kazi.
“Mkakati huu mmoja utasaidia
kurahisihsa kujenga mwamko wa uelewa kwani tatizo letu linafanana kwa
bara la Afrika ni suala zima la uwelewa wa masuala ya ukatili hivyo ni
jukumu letu sote kutoa elimu kwa wananchi wetu juu ya ukatili kwa watoto
na elimu ya saikolojia”alisema Dkta Kigwangala.
Kwa Upande wake Katibu mkuu wa
Afrika mashariki Balozi Leberat Mfumukeko amesema kuwa Jumuiya ina
mpango mkakati kwa kuzitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuhakiksha
wanazipa kipaumbele masuala ya watoto katika ustawi wa kijamii na
maendeleo ya bara hili ambapo watoto asilimia 50% wanaishi katika
mazingira hatarishi katika nchi za jumuiya hiyo.
Amesma kumekuwapo na mambo mbali
mbali yanayochangia watoto kukuwa wakikosa ushauri nasaha na wengine
wakikumbwa na ukatili kwa kukosa huduma za Afya lishe duni haki za
ustawi wa watoto sisi tukiwa na mip[ango ya kimaendeleo kama hatukuwapa
kipaumbe watoto hapo siku za usoni tutashuka kimaendeleo kwa kukosa
nguvukazi imara.
Nae mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa
Dodoma Fatma Tawfiq amesma kuwa ukosefu wa elimu ya jinsia kwa watoto
ikiwemo elimu ya Afya ya uzazi imechangia watoto kutoweza kuzifikia
ndoto zao na kuwataka wazazi barani Afrika kuanza kuwapa nafasi watoto
wao kuweza kujieleza hii itasaidia hata taifa kimaendeleo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi
wa taasisi ya REPSSI Bi Edwick Mapalala alisema kuwa mkutano huo
unawakutanisha wataalamu wa masuala ya watoto kutoka ndani ya serikali
za nchi 13 na wadau kutoka taasisi ziosizo za kiserikali mashirika ya
umoja wa mataifa na yale yanaohusika na masuala ya watoto pande zote za
ulimwengu lengo kuu ni kuelimishana na kufundishana katika kuhudumia na
kukabiliana na masuala mtambuka yahusuyo watoto.
SHARE
No comments:
Post a Comment