LILONGWE- POLISI
nchini, wametoa kibali cha kukamatwa kwa Rais wa zamani, Joyce Banda, kuhusiana
na sakata ya ulaji rushwa inayofahamika kama Cashgate wakati wa utawala wake.
Polisi wamesema
wamepata ushahidi wa kuaminika, kuhusiana na sakata hilo lililohusisha upotevu
wa dola za Marekani milioni 250 (sh bilioni 550).
Kashfa hiyo inaibua
uwezekano kwamba, huenda rais huyo wa zamani alitenda makosa yanayohusiana na
kutumia vibaya mamlaka na utakatishaji wa fedha.
Banda yuko
nje ya nchi na polisi wamesema wataomba msaada kutoka kwa polisi wa kimataifa
Interpol, kuhakikisha anarejea nchini kujibu mashtaka.
Cashgate
ndiyo sakata kubwa zaidi la ufisadi kuwahi kutokea katika historia ya Malawi.
Sakata hilo linahusisha
kuporwa kwa fedha za umma, wakati wa utawala wa Banda. Rais huyo wa zamani
hajazungumzia tuhuma hizo dhidi yake.
BBC.
SHARE
No comments:
Post a Comment