Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais,Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifungua Kikao cha
Wazi cha kupokea maoni ya wadau kuhusu dhamira ya Serikali kupiga
marufuku uzalishaji,uuzaji,usambazaji na matumizi ya mifuko ya plastiki
leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Prof. Faustine Kamuzora akiongea wakati wa ufunguzi wa Kikao hicho
leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais,Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.
Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akiongea wakati wa Kikao hicho mapema leo.
Mwenyekiti wa Umoja wa
wazalishaji wa mifuko isiyo na athari kwa mazingira Bw. Jumanne Mgude
akionesha mfuko unaozalishwa hapa nchini usio na athari kwa mazingira
wakati wa Kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Wande Printing and Packaging (T) Ltd Bw. Joseph Wasonga akitoa maoni ya
wamiliki wa Viwanda vya Kuzalisha mifuko ya plastiki hapa nchini wakati
wa kikao hicho.
Katibu wa Umoja wa wazalishaji wa
mifuko isiyo na athari kwa mazingira Bw. Sadick Mgonge akitoa maoni ya
umoja huo wakati wa Kikao hicho leo.
Sehemu ya wadau walioshiriki kikao hicho leo Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mjadala na maoni ya washiriki .
(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)
…………………………………………………………………………………………….
Frank Mvungi-Maelezo
Wadau wa Mazingira na
Wazalishaji wa Mifuko ya Plastiki hapa nchini wameipongeza Serikali kwa
kuwakutanisha pamoja ili kujadili kuhusu matumizi ya mifuko ya plastiki
na kutoa maoni yao kwa Serikali juu ya kuchukua hatua kwa mujibu wa
Sheria ya Mazingira.
Akizungumza wakati akifungua
kikao cha wazi cha kupokea maoni ya wadau kuhusu dhamira ya Serikali
kupiga marufuku uzalishaji, uuzaji, usambazaji na matumizi ya mifuko ya
plastiki, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Mhe. January Makamba amesema dhamira ya Serikali ni kupata maoni ya
wadau na wazalishaji wa mifuko hiyo ili Serikali ifanye tathmini kabla
ya kuchukua hatua na kuweka mazingira yatakayowezesha utekelezaji wa
Sheria ya Mazingira kwa kila mdau.
“Changamoto imekuwa kubwa katika
matumizi ya mifuko ya plastiki katika swala la mazingira kwani
tumeshuhudia miundo mbinu yetu ikiathirika, mifugo na hata viumbe vya
baharini na kwa mujibu wa tafiti kuna hatari baadae mifuko hii ikawa
mingi zaidi baharini kuliko samaki” Alisisitiza Makamba.
Akifafanua Makamba amesema kuwa
Serikali imeona ni vyema ikakutana na wadau ili ipate maoni yao kwa
kuzingatia kifungu cha 178 cha Sheria ya Mazingira kinachotaka wananchi
na wadau kushirikishwa na kupata taarifa kuhusu maswala ya mazingira.
Aliongeza kuwa kuanzia sasa Ofisi
yake itakuwa ikishirikiana na wadau katika mambo yote yanayohusu
mazingira ili kuongeza tija na kutoa fursa kwa wadau hao kutoa maoni
yatakayosaidia katika usimamizi wa Sheria na Kanuni.
Naamini kutakuwa na kuvumiliana
wakati wa kutoa maoni ili Serikali ipate maoni ya wadau wote kwa ufasaha
na hii itasaidia Serikali katika kuchukua hatua ikiwemo kuhakikisha
kuwa kuna usimamizi dhabiti wa Sheria ya Mazingira.
Pia Waziri Makamba alilitaka
Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kusimamia Sheria ya
Mazingira kikamilifu ili kulinda rasilimali za Taifa.
Kwa upande wake Naibu Mwenyekiti
wa Chama cha Wazalishaji wa Plastiki Tanzania Bw. Ahmed Abdallah
amepongeza utaratibu huo wa Serikali kukutana na wadau.
Kumekuwa na maoni mbalimbali
kuhusu matumizi ya mifuko ya plastiki huku baadhi ya wadau wakidai
imekuwa na athari kubwa katika mazingira zikiwemo magonjwa, uharibifu wa
miundo mbinu na kuleta mabadiliko ya tabia nchi .
SHARE
No comments:
Post a Comment