NA OWM, ILEJE
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh.
bilioni 1.669 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika wilaya ya Ileje
mkoani Songwe.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Julai 22, 2017) wakati
akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ileje katika ukumbi wa
Shule ya Sekondari Itumba.
Waziri Mkuu amesema kati ya fedha hizo sh. bilioni moja
zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji katika miji miwili ya Isongole
na Itumba wilayani Ileje.
“Kiasi kingine cha sh. milioni 669 kimetengwa kwa ajili ya maji
katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ileje katika mwaka wa fedha wa
2017/2018.
Hata hivyo, amesema Serikali inaendelea na utekelezaji wa
Kampeni ya Rais Dkt. Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kusogeza huduma
ya maji kwa urahisi.
Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi
katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama katika umbali
usiozidi mita 400.
Wakati huo huo Waziri Mkuu ameiagiza Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Mkoa wa Songwe kuhakikisha inaimarisha ulinzi katika maeneo ya
mipaka.
Amesema kamati hiyo inatakiwa kuimarisha ulinzi katika maeneo
yote ya mipaka ili kuizua wageni kuingia bila ya kufuata taratibu zilizowekwa
kisheria.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Bw. Joseph Mkude alisema katika
kipindi cha Julai 2016 hadi Juni 2017 jumla ya wahamiaji haramu 38 walikamatwa
kwenye wilaya hiyo.
Alisema kati ya wahamiaji hao haramu 36 ni raia wa Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) na wawili walikua raia wa Malawi na wote
walirudishwa makwao.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Ileje baada ya
kuwasili kwenye makazi ya Mkuu wa wilaya hiyo akiwa katika ziara ya mkoa
wa Songwe Julai 22, 2017.
Baadhi
ya watumishi wa umma, viongozi wa dini na taasisi binafsi wakimsikiliza
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao mjini Ileje Julai
22, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa
jengo la hospitali ya wilaya ya Ileje akiwa katika ziara ya mkoa wa Songwe,
Julai 22, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kushoto) wakitazama mbegu za mahindi
zinazozalishwa na Kikundi cha SAM cha Ileje wakati alipotembelea banda la
kikundi hicho kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye stendi ya mabasi ya
Ileje Julai 22, 2017.
SHARE
No comments:
Post a Comment