NA MWANDISHI WETU, MWANZA
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imesema
imeridhishwa na uwekezaji wa Kiwanda cha Nyama cha Chobo kilichombo Misungwi
jijini Mwanza kwa kuwa kinawahakikishia wakulima wadogo masoko ya mifugo yao.
Pongezi hizo zimetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa TADB, Bw. Francis Assenga wakati alipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya
uwekezaji wa miundombinu ya Kiwanda hicho.
Bw. Assenga amesema kuwa Kiwanda cha Chobo ambayo
inamilikiwa na kijana mzalendo, John Chobo ina uwezo mkubwa wa kusadia wakulima
wadogo kwa kununua mifugo yako hivyo kuwapatia fursa za masoko wakulima
hao.
“Miundombinu ya Kiwanda inaweza kuchinja zaidi ya
ng’ombe 600 kwa siku, hili ni soko kubwa sana kwa wakulima wadogo wa mikoa ya
Kanda ya Ziwa hali itakayounga mkono juhudi za serikali hasa TADB katika
kuboresha minyororo ya thamani kwenye sekta ya mifugo,” alisema.
Bw. Assenga amesema Serikali iliamua kuanzisha Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya
wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo
na kuchagiza mapinduzi katika kilimo nchini.
Bw. Assenga ameongeza kuwa sekta ya mifugo ni mojawapo
ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani
mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa ufugaji wa
ng’ombe wa nyama na maziwa nchini.
Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza
uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Ng’ombe wa Nyama na Maziwa.
“Benki inatoa mikopo na kusaidia uwekezaji kwa ajili
ya ujenzi, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya kuhudumia ng’ombe
ikiwemo majosho na mabwawa ya kunyweshea na pamoja na usindikaji wa nyama na
maziwa kwa ajili ya kuongeza thamani nyama na maziwa,” alisema Bw. Assenga.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mmiliki wa Kiwanda
hicho, Bw. John Chobo alisema kuwa kwa sasa kiwanda chake hakijafikia uwezo wa
kutumika kwa asilimia 100 kutokana na changamoto za kimtaji zinazomkabili na
alitumia fursa hiyo kuiomba Benki ya Kilimo kumuwezesha ili aweze kutoa ajira
zaidi kwa Watanzania.
Kwa mujibu wa Bw. Chobo kwa sasa kiwanda chake kina
wafanyakazi 85 na kikifikia uwezo wa kuzalisha kwa asilimia 100 kitaweza
kuajiri zaidi ya wafanyakazi 300 watakaofanya kazi kiwandani na 300 watakaokuwa
wakisimamia shamba.
“Tunaiomba TADB kutatulia changamoto za ukosefu wa
mitaji ya uhakika kwa kuwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za
fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa na ambayo riba yake
ni kubwa sana.,” alisema.
Meneja
Uendeshaji wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Charles Hotar akionesha mashine ya
kuchakatia nyama kwa ajili ya kutengenezea soseji kwa wageni kutoka Benki ya
Kilimo (hawapo pichani).
Mtaalamu
kutoka Idara ya Soseji wa wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Stanley Kirio akiendelea na
zoezi la kuandaa soseji.
Meneja
Uendeshaji wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Charles Hotar (kushoto) akionesha soseji
zilizokuwa katika hatua za ufungaji. Wanaomuangalia ni wageni kutoka Benki ya
Kilimo.
Mmiliki
wa Kiwanda cha Chobo Investment, Bw. John Chobo (kulia) akiwaonesha
vifungashio vya soseji zilizotayari kupelekwa sokoni. Wanaomtazama ni
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) na
Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha
(katikati).
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akionja soseji za Kiwanda cha
Chobo.
Mmiliki
wa Kiwanda cha Chobo Investment, Bw. John Chobo (mbele) akiwaongoza
viongozi wa Benki ya Kilimo kutembelea kiwanda hicho. Aliofutana nao ni Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) na Mkurugenzi wa
Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (kushoto).
Ugeni
kutoka TADB ukijionea nyama iliyohifadhiwa kwenye jokofu (chiller) kusubiri
kuchakatwa kabla kupelekwa sokoni.
SHARE
















No comments:
Post a Comment