Kaimu
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace John Karia
amempongeza Leodegar Chilla Tenga – Rais wa Heshima wa TFF kwa kuteuliwa
kuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Leodegar Chilla Tenga aliteuliwa
Ijumaa iliyopita katika Mkutano Mkuu wa CAF uliofanyika mjini Rabat
nchini Morocco ambako katika kamati hiyo muhimu, Rais wa zamani wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Zambia (FAZ), Kalusha Bwalya.
“Hii ni sifa kwa nchi. Na ni sifa
kwa Mheshimiwa Tenga. Tunajisikia fahari Tanzania kung’ara katika
medani za uteuzi katika vyombo vya kimataifa kama CAF. Uteuzi wake ni
kwamba anafungua njia kwa nchi na wengine ili kufanya vema,” anasema.
Karia amesema ana imani na Tenga
na Bwalya katika kamati yao kwa sababu ni wachezaji na manahodha wa
zamani wa timu za taifa. Itakumbukwa kwamba Tenga alikuwa akicheza kama
mlinzi Bwalya alikuwa mshambuliaji. “Wote ni wataalamu. wanajua,
tutafanikiwa.”
Katika mkutano huo mbali na
kuteua akina Tenga na kuunda kamati nyingine, pia ulifanya marekebisho
ya muundo wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na sasa
yatakuwa yakifanyika katikati ya mwaka badala ya mwanzoni mwa mwaka.
Kwa miaka ya nyuma hadi mwaka huu
ambako michuano hiyo ilifanyika Gabon, ilikuwa ikifanyika kuanzia
katikati ya Januari hadi Februari. Mbali na kuzitoa Fainali za AFCON
katikati ya mwaka hadi mwanzoni, pia idadi ya timu za kushiriki
zimeongezwa kutoka 16 hadi 24 ambako sasa utakuwa na timu washindwa 10
badala ya mbili kama ilivyokuwa awali.
“Watanzania wasikate tamaa, hata
kama kwa mfumo wa sasa unaofutwa au tuseme kubadilishwa, bado tuna
malengo yetu yalikuwa ni kufuzu, Tunajipanga kwa hali ya sasa na
hatujaanza vibaya na Lesotho. Bado tuna nafasi,” amesema Karia.
Michuano hiyo kuhamishwa kutoka Januari na Februari hadi Juni na Julai kuanzia Fainali za mwaka 2019 nchini Cameroon.
Hii si mara ya kwanza kwa Tenga
aliyepata kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika
Mashariki na Kati (CECAFA), bali amekuwa akiteuliwa mara kwa mara kuwa
Mjumbe wa Kamati mbalimbali za CAF. Hongera sana Rais wa Heshima wa TFF,
Leodegar Chilla Tenga.
SHARE
No comments:
Post a Comment