Rais wa Ufaransa
Manuel Macron amesema kuwa anaheshimu uamuzi wa rais Trump kujitoa
katika makubaliano ya tabia nchi ya Paris na kwamba Ufaransa itaendelea
na juhudi zake kuhusu makubaliano hayo.
Akizungumza pamoja na Macron, rais wa Marekani Donald Trump alisema kwamba huenda Marekani ikabadili msimamo wake lakini hakutoa maelezo ya zaidi.
''Kitu kitafanyika kwa heshima ya makubaliano ya Paris''.
Bwana Trump aliongezea: Tutaona kile kitakachofanyika.
- Afrika yamlaumu Trump kuupuza mkataba wa Paris
- Trump kutangaza msimamo wake kuhusu makubaliano ya Paris
- G20: Viongozi watofautiana na Trump kuhusu makubaliano ya Paris
- Mkataba wa Paris: Hatua ya Trump yawakera viongozi
Bwana Macron alisema kuwa ni muhimu kuweka makubaliano hayo kando huku viongozi hao wawili wakizungumza vile watakavyofanya kazi kuhusu maswala kama vile kusitishwa kwa mapigano nchini Syria na ushirikiano wa kibiashara.
Tuna tofauti zetu; Bwana Trump ana ahadi za uchaguzi alizowapatia raia wa tafa lake na pia mimi nilikuwa na ahadi, je vitu hivi vinapaswa kuturudisha nyuma katika maswala yote? Hapana, alisema Macron.
Bwana Macron na Trump baadaye walizungumza kuhusu juhudi za pamoja za mataifa hayo katika kukabiliana na ugaidi na hususan kundi la wapiganaji wa Islamic State nchini Syria na Iraq.
"Marekani inahusishwa pakubwa katika vita vinavyoendelea nchini Iraq'', alisema Macron, ''ningependa kumshukuru rais kwa kila kitu kinachofanywa na wanajeshi wa Marekani katika eneo hili''.
''Tumekubaliana tuendeleze na juhudi zetu za pamoja'' ,aliongezea ''husuasan mipango baada ya vita''.
Bwana Macron alisema kuwa Ufaransa itaweka mikakati kadhaa ili kusaidia kuimarisha uthabiti katika eneo hilo
SHARE
No comments:
Post a Comment