
Ikulu ya
White House imesema kuwa Rais Donald Trump, anaunga mkono makubaliano
yasiopendelea upande wowote yaliyoafikiwa katika bunge la Congress ya
kuiwekea vikwazo Urusi. Imesema kuwa Rais Donald Trump, anaunga
makubaliano yasiopendelea upande wowote yaliyoafikiwa katika bunge la
Congress ya kuiwekea vikwazo Urusi.Afisa habari wa Ikulu ya White House
Sarah Huckabee-Sanders anasisitiza kuwa, licha ya hatua hiyo awali white
house ilipinga mswada wa uamuzi huo, japo kuwa kwa sasa inafurahia
mswaada wa mwisho uliopitishwa.
Putin amekana nchi yake kuhusika kuingilia uchaguzi huo

Bunge la
Congress linataka Urusi iadhibiwe kwa madai ya kuingilia uchaguzi wa
urais uliofanyika mwaka jana nchini Marekani.Bunge hilo linatarajiwa
kupiga kura hapo kesho siku ya jumanne kupitisha muswada huo kuwa sheria
inayoitaka ofisi ya Rais kutoingilia mwenendo wa hatua za kidplomasia
dhidi ya Moscow.Ikulu ya white house hata hivyo imekuwa na kauli
zinazotofautiana mara baada ya msimamo wa bunge la Congress katika
vikwazo vipya dhidi ya tuhuma za Urusi.
Kupitishwa
kwa sheria hiyo na bunge la congress kutamnyima uwezo Rais Trump,
kuondoa kikwazo chochote kitakachopitishwa dhidi ya Urusi.
Urusi imeendelea kupinda shutuma za kuingilia uchaguzi huo.
CHANZO-BBC SWAHIL
SHARE
No comments:
Post a Comment