
Rais
Magufuli jana Julai 24, 2017 ameweka jiwe la msingi katika miradi mikubwa
miwili; mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Tabora, Igunga na Nzega
pamoja na mradi wa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa ndege wa Tabora na
kufungua barabara mbili za Tabora – Nyahua na Tabora – Puge –
Nzega.Niwaombe viongozi Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi
musimamie kero za Wananchi.
Muwe mnakaa angalau kwa kila wiki kila
kiongozi katika mahali alipo wasimamie matatizo ya wananchi. Matatizo ya
Wananchi ni mengi wanashindwa kuvumilia wanaona Rais pekee ndiye
anaweza akatatua yale matatizo.
Niwaombe sana kuanzia Mkuu wa Mkoa,
Mawaziri, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi muwe mnashughulikia matatizo na
kuyamaliza.
“Nitakuwa
natembelea mikoani nitakapokuwa napewa matatizo na matatizo hayo yawe
yalikuwa chini ya uwezo wa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi,
Katibu Tarafa, Mwenyekiti wa Kijiji kuyatatua na hakutatua, mimi nalala
mbele na huyo kiongozi.” – Rais Magufuli.
SHARE
No comments:
Post a Comment