Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Baada
ya Matokeo ya Kidato cha Sita , Global Education Link (GEL) ambao ni
mawakala wa Vyuo Vikuu vya Nje imesema kuwa wanafunzi wanaotaka kujiunga
na vyuo vikuu vya nje udahili ni papo kwa papo na vyuo hivyo viko wazi.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link
(GEL), Abdulmalik Mollel amesema katika azma ya serikali ya awamu ya
tano ya viwanda, inahitaji rasilimali watu ya kutosha ambao ndio
watasukuma gurudumu hilo la viwanda na ujuzi upo katika vyuo vya nje
ambapo nchi zenye vyuo vina uatajiri wa viwanda.
Mollel
amesema kuwa vyuo ambavyo anashirikiana na vina uwezo wa kutosha katika
uzalishaji wa rasilimali watu katika sekta ya viwanda.Amesema kuwa
wazazi wanaotaka kupeleka wanafunzi katika vyuo vikuu vya nje
hawatajutia kutokana na mazingira wanayokwenda kusoma huko.
Mollel
amesema kuwa wazazi na wanafunzi wafike katika ofisi zao ziko katika
mikoa ya Dar es Salaam viwanja vya Saba saba , Dodoma , Mbeya, Mwanza,
Zanzibar, Arusha pamoja na nchi ya Zambia.
Amesema
kuwa mwanafunzi atayekuwa anapitia katika wakala hiyo atapata uangalizi
kwa muda wote masomo yake katika kuhakikisha mzazi kile anachokifanya
kwa kijana wake hawezi kujutia.
Mollel
amesema kuwa wazazi na wanafunzi wanaweza kufika katika ofisi zao kwa
maelezo na jinsi kuwafanyia udahili wa papo kwa papo.
Mkurugenzi
wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akizungumza na wateja
waliofika kupata huduma katika ofisi za Global Education Link zilizopo
katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa
Masoko wa Global Education Link (GEL) Damaricy Peter akiwapa maelekezo
wateja waliofika kupata huduma katika ofisi za Global Education Link
zilizopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa
wa Hati ya Kusafiria Passport , Abdul Milanzi akimsainisha fomu ya hati
ya kusafiria mteja wa Global Education Link GEL jana katika ofisi za
Global Education Link zilizopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es
Salaam.
Meneja
Masoko wa Chuo Kikuu cha Lovely Professional, Love Kumas akizungumza na
mteja katika ofisi za Global Education Link (GEL) jana jijini Dar es
Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
SHARE
No comments:
Post a Comment