Timu ya taifa ya
Ujerumani imetwaa taji la kombe la mabara baada ya kuishinda Chile kwa
bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Saint Petersburg
nchini Urusi.
Katika mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu Ureno walifanikiwa kutwaa medali ya shaba baada ya kuichapa Mexico kwa mabao 2-1.
Beki wa Ureno Luis Neto aliwapa Mexico goli la kuongoza baada ya kujifunga katika dakika ya 55, kabla ya Pepe kuzawazisha goli hilo katika dakika za lala salama.
Bao la mkwaju wa penati lilifungwa na Adrien Silva katika dakika ya 104 likawapa Ureno ushindi muhimu licha ya kumkosa nyota wake Cristiano Ronaldo.
CHANZO: DW
SHARE
No comments:
Post a Comment