
Na. Bushiri Matenda na Immaculate Makilika- MAELEZO
Waatalaam wa Mpango wa
Kijitathmini Kiutawala Bora Barani Afrika (APRM) wameelezea
kuridhishwana Serikali ya Rais John Pombe Magufuli katika kusimamia
misingi ya Demokrasia na UtawalaBora nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Tathmini za
Nchi katika Sekretariati ya APRM na Mratibu wa Mchakato wa Tanzania,
Dkt. Rachel Mukamunana alitoa kauli hiyo leo jijini Dar es Slaam wakati
akiongea na waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa ripoti ya APRM
utakaofanywa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Rachel alisema kuwa serikali
ya Tanzania imekuwa ikitoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa
masuala yanayohusu utawala bora ikiwemo kutatua kero mbalimbali
zikiwemo zile zinazohusu masuala ya muungano.
“Serikali ya Rais Magufuli
imeonesha kujitoa kwa dhati katika kusimamia masuala ya utawala bora na
uzinduzi wa ripoti hii ni kiashara tosha cha dhamira ya serikali katika
kusimamia misingi ya utwala bora”, alieleza.
Kutoka na kujitoa huko kwa
seriklai, Dkt. Rachel alisema kuwa anatarajia serikali ya Tanzania
itaendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizoanishwa katika ripoti
hiyo ya mwaka 2012 ambayo inayotarajiwa kuzinduliwa kesho (leo).
Nae Katibu Mtendaji wa APRM
Tanzania, Rehema Twalib alieleza kuwa ripoti hiyo imeanisha sifa ambazo
Tanzania imekuwa ikisifiwa nazo kuwa ni pamoja na kudumisha amani na
umoja, kudumisha Muungano kwa zaidi ya miaka 50, pamoja na uboreshwaji
wa utoaji huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, maji, usawa wa kijinsia
na Teknolojia na habari na mawasiliano (TEHAMA).
Alibainisha sifa zingine
linazotajwa kwa Tanzania kuwa ni kulinda haki binadamu, matumizi ya
lugha moja ya kiswahili, na hatua za maendeleo ya kiuchumi nchini.
Katibu huyo alisema kuwa uzinduzi
wa ripoti ni utekelezaji wa mojawapo ya matakwa ya kiutaratibu katika
mchakato wa APRM, ikiwa ni kiashiria kimojawapo cha utekelezaji rasmi ya
yale yaliyoandikwa kwenye ripoti pia kielelezo cha utayari wa
Serikali katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wake.
Rehema alisema kuwa lengo la APRM
ni kuzisaidia nchi za Kiafrika, Tanzania ikiwa mwanachama mmoja wapo,
kuhakikisha kuwa zinaimarisha utawala bora. Hii ni kwa kuwashirikisha
wananchi wao kubanisha changamoto ili kuzigeuza kuwa fursa za maendeleo
na mambo mazuri ya kuendelezwa kwa faida ya nchi yenyewe na hata kuwa
mfano wa kuigwa na nchi nyingine.
APRM Tanzania ilipewa dhamana na
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusimamia majukumu ya nchi
katika kuratibu tathimini ya Utawala bora kwa mujibu wa wa miongozi ya
Wakuu wa Nchi za Kiafrika.
SHARE








No comments:
Post a Comment