Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, HusseinMansour
(hayupo pichani), alipotembelea banda la Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia (COSTECH), kwenye Maonyesho ya Nanenane viwanja vya Ngongo
mkoani Lindi leo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima
Dendegu. Maonyesho hayo yatafungwa na Makamu wa Rais mchana.
Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, HusseinMansour (kushoto), akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, alipotembelea banda la COSTECH.
Mtafiti kutoka COSTECH, Bestina Daniel, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la COSTECH katika maonyesho hayo.
Mtafiti
kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Mikocheni (MARI), Christina
Kidulile, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la COSTECH
jinsi ya kuotesha mimea kwa kutumia chupa.
Mratibu
wa Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Philbert Nyinondi, kushoto
akizungumza na wadau wa kilimo jinsi Maktaba ya Taifa ya Sokoine ya
Kilimo-SNAL itakavyowawezesha wakulima wa Tanzania kupata taarifa za
kilimo kwa njia rahisi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kudhibiti
Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Patric Ngwediage (wa nne kulia), akiwa
na Crew nzima ya COSTECH katika banda hilo.
Mtafiti
kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro,
Ismail Ngolinda, akitoa maelekezo kwa wakulima jinsi ya kuotesha miche
kwa njia ya chupa.
SHARE
No comments:
Post a Comment