Mgeni
rasmi katika kilele cha Maonyesho haya alikuwa waziri wa ofisi ya Rais
tawala za mikoa na serikali za Mitaa MHE. George B. Simbachawene
akimkabidhi mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah tuzo ya mshindi wa
tatu sambamba na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Aloyce
Kwezi.Katikati
DC wa kilolo Asia Abdallah , kushoto aliyeshika hati, Mkurugenzi
Halmashauri ya Kilolo Aloyce Kwezi na mwishoni kwa Mkurugenzi ni Dkt.
Mwingira Afisa Mifugo mkuu Wilaya na kulia ni Afisa Kilimo
mkuu Wilaya ndgu. Kuziwa..
Na Fredy Mgunda, Mbeya
Halmashauri
ya wilaya ya Kilolo mkoani iringa imeshika nafasi ya tatu katika
maonyesho ya nane nane ambao huhusisha maswala ya kilimo yaliyofanyikia
jijini mbeya kwa kanda ya nyanda za juu kusini na kuhudhuliwa na
viongozi mbali mbali kutoka mikoa yote ya nyanda za juu kusini.
Akizungumza
mara baada ya kupokea zawadi ya kuwa washidi wa tatu wa maonyesho hayo
ya nane nane mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah aliwapongeza
wananchi na viongozi wa wilaya hiyo kwa kufanya vizuri katika maonyesho
hayo kwa kile walichokifanya na kuonyesha kuwa Kilolo Kilimo kinasaidia
kuinua kipato kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
"Mimi
niwashukuru sana kwa zawadi waliyotupa wananchi na viongozi wa Wilaya
ya Kilolo maana ushindani ulikuwa mkubwa mno hasa ukiangalia wilaya zote
za nyanda za juu kusini zinasifika sana kwa Kilimo cha mazao mbalimbali
na ufugaji hivyo haikuwa rahisi sana kufika hapa mwaka huu"alisema
Abdallah
Abdallah
alisema kuwa atakaa na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo
Kupanga mikakati madhubuti ili mwakani waweze kushika nafasi ya kwanza
na kuwa wilaya ya mfano huku nyanda za juu kusini hata Tanzania kwa
ujumla.
"Sasa
kazi imeanza na nitahakikisha kila kitu mwakani kitakuwa vizuri na
tutafanya vizuri sana kwa kuwa halmashauri ya wilaya ya Kilolo ina
maeneo mengi mazuri ya uwekezaji kwenye sekta ya Kilimo na ufugaji hivyo
lazima tutatafuta njia mbada ya kuinua Kilimo cha wilaya ya Kilolo"
alisema Abdallah
Aidha Abdallah alisema mikakati yake ni kuboresha pale walipokwama ili kupata matokeo chanya katika maonyesho yajayo.
"Mikakati
iliyopo ni kwamba mwisho wa maonesho haya ndiyo mwanzo wa maonesho
mengine, tumegundua vitu vilivyotufanya kuwa namba tatu ni pamoja na
ubunifu, hivyo tutazidi kuwa wabunifu kwa maonesho yajayo ili tufikie
ushindi mnono zaidi" alisema Abdallah
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo Aloyce Kwezi
alisema kuwa halmashauri inamikakati mingi ya kuboresha maeneo ya Kilimo
kuwaomba wadau mbali mbali wanaotaka kuwekeza kwenye Kilimo wafike
katika ofisi halmashauri ili kujadiliana namna ya uwezaji na maeneo
wanayoweza kuwekeza.
"Halmashauri
ya wilaya ya Kilolo ina maeneo mengi mazuri kwa ajili ya Kilimo ambayo
bado hayafanyiwa Kilimo hivyo naomba wadau wenye nia ya kuwekeza kwenye
Kilimo waje kuweza maana maeneo ni rafiki kwa Kilimo cha aina yoyote ile
kutokana na hali ya hewa iliyopo huku" alisema Kwezi
Naye
afisa mifugo mkuu wa wilaya ya kilolo Dkt. Mwingira aliupongeza uongozi
wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo kwa jitihada za kuinua Kilimo na
ufugaji kwa wananchi wa Wilaya hiyo na ndio sababu kubwa kupata
mafanikio ya kushika nafasi ya tatu katika maonyesho ya nane nane.
"Mimi
nampongeza sana Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi kwa ubunifu wao
ambao umetusaidia kufika hapa hivyo naomba tuwape ushirikiano katika
kukuza Kilimo cha Wilaya ya Kilolo "alisema Dr mwingira
Katika maonyesho hayo Mgeni
Rasmi alikuwa Waziri ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa
George Simbachawene na huku nafasi ya kwanza ilichukuliwa na
halmashauri ya Mpanda na nafasi ya pili ilishikwa na Tunduru.
SHARE
No comments:
Post a Comment