TRA

TRA

Tuesday, August 8, 2017

HII NDIYO NIDA. HAPA MAOFISA WAKIMPOKEA MAKAMU WA RAIS

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Banda la maonyesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Makamu wa Rais alipokelewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Rose Mdami

Makamu wa Rais anapokea taarifa ya shughuli za Usajili ambazo zimekuwa zikifanyika katika Banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakati wa Maonyesho ya Nanenane kwenye Viwanja vya Ngongo – Lindi.
Makamu wa Rais akikagua Vitambulisho vinavyogawanywa kwa wananchi Wananchi wakati wa maonyesho ya Nanenane mkoani Lindi.

Mhe. Makamu wa Rais akikagua fomu za Usajili zinavyohakikiwa kabla ya mwananchi kuchukuliwa alama za Vidole, Picha na Saini ya Kielektroniki.
Makamu wa Rais akikagua mashine za Usajili zinazotumika kuwasajili wananchi; ikiwemo uchukuaji wa alama za kibaiolojia, Picha na Saini ya Kielektroniki
Watumishi wa NIDA wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupata ushindi kwenye maonyesho ya Nanenane kwa mwaka 2017.

……………………….

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametembelea banda la Maonyesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na kufurahishwa na ufanisi mkubwa katika kuunganisha mifumo ya Serikali yenye kulenga utoaji huduma bora na kurahisisha shughuli ya Utambuzi kwa wananchi.

Mheshimiwa Makamu wa Rais ametembelea Banda la NIDA akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele cha maonyesho ya sikukuu ya Wakulima Kitaifa maarufu Nanenane yaliyofanyika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi. Mhe. Samia aliambatana na viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Dr. Charles Tizeba.

Katika maonyesho hayo NIDA ni miongoni mwa Taasisi zilizofanya vizuri na kupata ushindi katika makundi 15 yaliyotangazwa.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger