
Mabingwa
watetezi wa Kombe la FA CUP timu ya Arsenal imenyakuwa kombe la Ngao ya
Hisani baada ya kuwalaza Chelsea kwa jumla ya Penalti 4-1 kutokana na
dakika 90 kumalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.Kipindi cha kwanza
kilikuwa kigumu kwa pande zote mbili baada ya milango yote kushindwa
kufungana huku Arsenal wakipata pigo baada ya Nahodha Per Mertesacker
aliyechanika kwenye uso wake wa jicho baada ya kugongana na Cahil wakati
wakiruka juu na nafasi yake kuchukuliwa na Kolasinac.

Kipindi cha pili kilianza kwa Chelsea kupata bao dakika ya 48 likifungwa na mchezaji wa Nigeria Moses

Kunako
dakika ya 84 kiungo mshambuliaji wa Chelsea Pedro kuoneshwa kadi
nyekundu moja kwa moja baada ya kumchezea vibaya Elneny na Xhaka kupiga
faulo na kumkuta beki wa pembeni Kolasinac kusawazisha kwa kichwa hadi
dakika 90 timu hizo zilitoka sare ya 1-1 na kupelekea kwenda matuta.


Wachezaji
walioweza kupata Penalti kwa upande wa Arsenal ni
Walcott,Monreal,Oxlade-Chamberlain na Giroud huku Chelsea bao lao
likifungwa na Cahill,huku Courtois na Morata wakikosa
VIKOSI VILIVYOANZA:
Arsenal: Cech, Holding, Mertesacker, Monreal, Bellerin, Elneny, Xhaka, Oxlade-Chamberlain, Welbeck, Iwobi, Lacazette.
Subs: Giroud, Ospina, Walcott, Maitland-Niles, Kolasinac, Nelson, Joseph Willock.
Chelsea: Courtois, Azpilicueta, Luiz, Cahill, Moses, Fabregas, Kante, Alonso, Willian, Pedro, Batshuayi.
Subs: Caballero, Rudiger, Morata, Musonda, Christensen, Scott, Boga.
SHARE








No comments:
Post a Comment