Magari ya viongozi wa Tume ya Uchaguzi yakiingia ukumbini hapo.
Maafisa
wakuu wa serikali pamoja na mabalozi wameanza kuwasili ukumbi wa Bomas
ambako kuna kituo cha taifa cha kujumlishia na kutangazia matokeo ya
urais, ishara kwamba tangazo muhimu linasubiriwa.
Ukumbi ukiwa umeandaliwa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohammed na washirika wengine wakuu wa Rais Uhuru Kenyatta wamewasili Bomas.
Viongozi wakiwasili.
Mabalozi
wa Marekani na Uingereza pia wamewasili. Kunashuhudiwa shughuli nyingi
na usalama umeimarishwa pamoja na hali kuonekana kubadilika katika
ukumbi huo.
Hali ilivyo nje ya ukumbi huo.
Tume ya
uchaguzi IEBC ilikuwa imetangaza kwamba inatarajia kupokea matokeo yote
kutoka vituo vya kupigia kura kufikia leo saa sita mchana.
Ukumbi
Mwenyekiti wa tume hiyo anatarajiwa kutangaza matokeo baadaye baada ya kuhakikiwa kwa fomu za matokeo.
Matokeo
ya awali kwenye tovuti ya tume hiyo yanaonesha Rais Kenyatta akiongoza
kwa takriban asilimia 10 ya kura zilizohesabiwa dhidi ya Bw Odinga.
SHARE
No comments:
Post a Comment