Benki Kuu ya Tanzania imetoa
leseni kwa kampuni mpya ya kutoa mikopo ya nyumba inayoitwa “First
Housing Company (Tanzania) Limited”.
Taarifa iliyotolewa na Idara ya
Sera na Leseni katika Kurugenzi ya Usimamizi wa Mabenki imeeleza kwamba
leseni hiyo inaipa nafasi kampuni hiyo mpya kufanya biashara ya kutoa
mikopo ya nyumba nchini. Makao makuu ya kampuni hiyo ni jijini Dar es
Salaam.
Hii ni mara ya kwanza kwa Benki Kuu kutoa leseni kwa kampuni ya mikopo ya nyumba nchini.
Benki Kuu pia inatoa leseni na
kusimamia benki, taasisi za fedha, maduka ya kubadilisha fedha, kampuni
za karadhana zinazotunza kumbukumbu za ukopaji za wananchi (credit
reference bureaus).
SHARE
No comments:
Post a Comment