
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya
Uingereza timu ya Chelsea hatiamaye Leo wamezinduka na kupataa ushindi
jumla ya magoli 2-1 dhidi ya Tottenham Spurs mchezo uliochezwa kwenye
dimba la uwanja wa Wembley ambao unatumiwa na Spurs.
Magoli
yote mawili ya Chelsea yamefungwa na beki wao Marcos Alonso huku bao la
wenyeji likifungwa na Michy Batshuayi aliyejifunga katika harakati ya
kuokoa krosi iliyopigwa kuelekea langoni mwa Chelsea hadi mpira
unamalizika Chelsea wameibuka na ushindi wa 2-1 baada ya mchezo wa
ufunguzi kufungwa na Burnely 3-1.








SHARE








No comments:
Post a Comment