TRA

TRA

Tuesday, August 15, 2017

DAWASCO KUKATA MAJI KUANZIA AGOSTI 14-19, 2017

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

TAARIFA KWA UMMA: DAWASCO KUKATA MAJI KUANZIA AGOSTI 14-19, 2017





UBORESHAJI WA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI WA RUVU CHINI
BAGAMOYO MKOANI PWANI.
Shirika la MajiSafi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia wateja wake wote wa Mji wa Bagamoyo Mkoani Pwani kuwa mtambo wa uzalishaji Maji wa Ruvu Chini utakuwa kwenye maboresho kwa wastani wa siku 5, kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 14/08/2017 hadi 19/08/2017, hivyo kusababisha baadhi ya maeneo ya Mji wa Bagamoyo kuwa na upungufu wa kiwango cha huduma ya Majisafi.
Sababu ya upungufu wa Majisafi: Maboresho ya Mtambo na mabomba makuu ya usafirishaji na usambazaji Maji.Maeneo yatakayoathirika: Mji Wa Bagamoyo Vijiji Vya Zinga, Mlingotini, Kilomo na Mapande.
Dawasco inawaomba wateja kutunza Maji ya kutosha kuepuka adha itakayojitokeza.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia: 

Kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (BURE) au
Dawati la huduma kwa wateja Dawasco Bagamoyo 0743 451 887
www.dawasco.go.tz 
Imetolewa Na:
Ofisi Ya Uhusiano
Dawasco-Makao Makuu.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger