Meneja
Uhusiano wa DAWASCO, Bi Everlasting Lyaro akitoa elimu juu ya matumizi
ya mfumo wa DAWASCO kwa kwa njia ya simu kwa watumiaji wa vyombo vya
Moto hususani Bajaj na Pikipiki katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar
es salaam. Mfumo huo umezinduliwa rasmi ili kutoa nafasi kwa wananchi
kupata na kutoa taarifa sahihi za DAWASCO.
Mmoja
ya waendesha bodaboda akimuuliza swali Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi.
Everlasting Lyaro juu ya matumizi ya mfumo mpya wa DAWSCO katika utoaji
na upatikanaji wa taarifa.
Mwendesha bajaji akihojiwana ITV juu ya matumizi ya mfumo mpya wa DAWASCO katika utoaji na upatikanaji wa taarifa.
Meneja
Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amewataka wananchi wa Dar
es Salaam na Pwani kupakua mfumo huu kwani ni rahisi kuutumia na hauna
gharama zozote. Anasema ni mfumo ambao utamrahisishia mteja kupata
taarifa muhimu zinazohusu huduma ya maji zikiwamo ankara ya mwezi,
taarifa za lini mteja alifungiwa huduma ya maji, muda ambao alifanya
malipo, lini mita yake ya maji ilisomwa na taarifa nyingine nyingi.
“Nawasihi
wateja wetu na wananchi wote kupakua mfumo huu mpya katika simu zenu za
mkononi ili kuweza kufurahia huduma zetu, hakuna gharama zozote ambazo
utatozwa. Kupitia mfumo huu utaweza kupata taarifa zote muhimu za huduma
ya majisafi zikiwemo taarifa za mivujo ya maji na ankara za maji za
kila mwezi,”amefafanua Bi. Lyaro.
Amesema
kwa sasa Wateja hawana haja ya kutumia muda mrefu katika ufuatiliaji wa
kuunganishwa huduma ya maji, bali kilichorahisishwa ni mteja kuweka
taarifa zake sahihi kwenye mfumo huo na DAWASCO.
SHARE
No comments:
Post a Comment