Naibu
Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mheshimiwa Bi. Mgeni Hassan Juma
Akizungumza na Wanawake wa Kikundi cha Vital Voices Grow Kutoka Nchi za
Kusini mwa Bara la Afrika Mjini Unguja.
Kikundi
cha Vital Voices Grow (VVGrow) kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la
Sahara (Sub-Saharan Africa) kwa mwaka 2015/2016 kimemtembelea
Mheshimiwa Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mheshimiwa Bi. Mgeni
Hassan Juma katika ofisi zake mjini Unguja, Zanzibar.
Kikundi
hicho kilichokuwa na ujumbe wa watu sita wakiongozwa na mwenyeji wao
Bi. Shekha Nasser ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Shear Illusions na
muasisi wa vipodozi vya Manjano walipata fursa ya kumtembelea Naibu
Spika kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya kumuwezesha
mwanamke kiuchumi.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mheshimiwa Bi. Mgeni Hassan Juma Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Wanakikundi hao. Mheshimiwa Bi. Mgeni ni Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa Unaibu Spika katika historia ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Katika ziara hiyo, VVGrow pia walipata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo wanawake na maendeleo ya kiuchumi kutoka kwa Bi. Mgeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wabunge Zanzibar (UWAWAZA). Pia ilikuwa ni fursa kwao kuonesha heshima yao kwa viongozi wa wanawake ambao wanaboresha ulimwengu na kuhamasisha usawa.

cha VVGrow kiko mjini Zanzibar kwa lengo la kujumuika na pia
kutathmini na kujadili mawazo ambayo yatawasaidia kukua kwa wanakikundi
wao binafsi na pia kukuza biashara zao kwa kujenga ajira na kukuza
uchumi.
VV
GROW Fellowship ni fursa kwa wanawake ulimwenguni wenye ushindani
mkubwa wa mafunzo ya mwaka mmoja wenye lengo la kusaidia wanawake
wamiliki wa biashara ndogo ndogo na za kati katika mataifa ya Amerika
Kusini na Caribbean, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, na Afrika
kusini mwa Sahara.
SHARE
No comments:
Post a Comment