TRA

TRA

Monday, August 14, 2017

HAKUNA VIBALI KWA AJILI YA KUUZA SHEHENA YA VIROBA ILIYOBAKI- MAKAMBA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Temani ambayo wana  ghala la kuhifadhia vinywaji aina ya viroba lililoko Kimara Temboni Bibi Elizabeth Massawe (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara yake ya kutembelea ghala hilo.
2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea ghala la kuhifadhia vinywaji la Kampuni ya Temani lililopo Kimara Temboni.
3
Sehemu ya vinywaji aina ya viroba na vifungashio vilivyopo katika ghala la kuhifadhia vinywaji la Kampuni ya Temani.
…………………………….
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amesema kuwa Serikali haina mpango wa kutoa vibali kwa ajili ya kuuza shehena ya kinywaji aina ya viroba vilivyopo stoo kwenye maghala ya Wafanyabiashara wa pombe hiyo.
Aliongea hayo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza katika ghala la  kampuni ya usambazaji wa vinywaji aina ya kiroba ya Temani iliyopo Kimara Temboni jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa Serikali ilitoa muda mrefu  kuanzia mei 2016 mpaka machi 2017 kwa wenye shehena hiyo ya viroba kuuza na kumaliza mzigo wote uliopo stoo hivyo basi baada ya Serikali kupiga marufuku pombe hiyo, hakuna kibali kitakachotolewa kwa ajili ya kuuza shehena ya mzigo wa viroba uliobaki. Akiongea  kwa Mh. Waziri , Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bi Elizabeth Massawe alisema wanaiomba Serikali iwasaidie ili waweze kupunguza mzigo mkubwa wa viroba ambao wanao katika ghala lao sababu wanapata hasara kubwa na wanatakiwa kulipia kodi ya magahala waliyokodi. .
Katika ziara hiyo ya kutembelea ghala la vinywaji la kampuni ya Tema Enterprise Waziri alikuta shehena kubwa ya katoni 150,000 za viroba  zilizofungashiwa katika vifuko vya plastiki.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger