
Mhandisi Mshauri wa barabara ya
Mayamaya – Mela (km 99.35), Eng. Leornado Licari, akitoa maelezo ya
mradi wa barabara hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (wapili kushoto),
alipofanya ukaguzi mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, akitoa
maelekezo kwa mkandarasi wa kampuni ya CHICO anayejenga sehemu ya
barabara ya Mayamaya – Mela (km 99.35), alipofanya ukaguzi mkoani
Dodoma.

Muonekano wa sehemu ya juu ya daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205 linalounganisha wilaya ya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga,
akikagua kingo za daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205
linalounganisha wilaya ya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (wapili
kushoto), akiwa na wataalamu wanaosimamia ujenzi wa barabara ya
Mayamaya – Mela (km 99.35), inayojengwa kwa kiwango cha lami mara baada
ya kuikagua mkoani Dodoma. Wanne kushoto ni Mkurugenzi wa barabara Eng.
Ven Ndyamukama.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga,
akikagua sehemu ya barabara ya Mela – Bonga (km 88.8), inayojengwa kwa
kiwango cha lami mkoani Manyara.

Ujenzi wa barabara ya Dodoma – Babati kwa kiwango cha lami sehemu ya Mela – Bonga (km 88.8), ukiendelea.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, akitoa
maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Manyara,
Eng. Bashiri Rwesingisa (kulia), na mkandarasi wa Kampuni ya China
Railway Seventh Group Co. Ltd anayejenga sehemu ya Mela – Bonga (km
88.8), mkoani Dodoma.
……………………..
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga,
amewaagiza Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma na
Manyara kuhakikisha wanatafuta eneo la kujenga kituo cha mizani ili
kudhibiti madereva wanaozidisha uzito katika barabara ya Dodoma- Babati
(km 263), inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Akizungumza katika eneo la
Bonga, mkoani Manyara Eng. Nyamhanga, amesema kuwa barabara hiyo ambayo
inatarajiwa kukamilika baadae mwezi huu inahitaji uwepo wa mizani kwa
haraka ili kudhibiti magari yanayozidisha uzito na kuharibu barabara.
“Hakikisheni mnatafuta eneo la kujenga mizani ndani ya
miezi miwilli ambapo wakandarasi bado wapo hapa ili iwe rahisi kwenu
kumtumia mmoja wa wakandarasi hawa kuweza kujenga kituo hiki haraka,
uwepo wa mizani hii utasaidia kudhibiti magari makubwa yanayozidisha
uzito”, amesema Katibu Mkuu Nyamhanga.
Aidha, Eng. Nyamhanga amewaagiza
mameneja wote nchini kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu wote
wanaopitisha mifugo katika barabara ili kudhibiti uharibifu wa barabara.
Amewataka madereva wote nchini kuendesha magari yao kwa
tahadhari na kuzingatia alama za barabarani ili kudhibiti ajali
zinazoepukika.
Katibu Mkuu Nyamhanga ametoa wito
kwa wananchi wanaoishi kando ya barabara hiyo kuhakikisha wanatumia
fursa ya kukamilika kwa barabara hiyo kwa ajili ya kuleta maendeleo
katika maeneo yao ili kukuza uchumi kwa familia zao na Taifa kwa ujumla.
Amemataka mkandarasi wa sehemu ya
barabara ya Mela – Bonga (km88.8) kuhakikisha anakamilisha kazi
zilizobaki kwa wakati na kwa viwango vilivyo kwenye mkataba.
Katika hatua nyingine, Eng.Nyamhanga, ametembelea na kukagua
barabara ya Mayamaya- Mela (km 99.35) kwa kiwango cha lami na daraja la
Kelema lenye urefu wa mita 205 na kuridhishwa na ujenzi wake na kumtaka
mkandarasi wa mradi huo kukabidhi mradi huo ifikapo mwezi Oktoba mwaka
huu.
Kwa upande wake, Mhandisi Mshauri
wa barabara ya Mayamaya- Mela (km 99.35), Leornado Licari,
amemhakikishia Katibu Mkuu huyo kumaliza mradi huo kwa wakati kwani
kazi zilizobaki kwa sasa ni ndogo kama kumaliza tabaka la mwisho la
lami na uwekaji wa alama za barabarani.
Barabara ya Dodoma- Babati (km
263) ni sehemu ya barabara kuu ya kaskazini (Great North road),
inayoanzia Capetown nchini Afrika Kusini hadi Cairo nchini Misri ambapo
hapa nchini barabara hiyo inayopitia Tunduma mkoani Mbeya, hadi Namanga
mkoani Arusha ina urefu wa kilomita 1500,hivyo kukamilika kwa sehemu ya
barabara ya Dodoma – Babati (km 263), kunaiunganisha barabara yote
kutoka Capetown hadi Cairo yenye urefu wa kilomita 100000 kwa kiwango
cha lami.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
SHARE








No comments:
Post a Comment