Meneja wa Mwalimu Commercial Bank, Plc,
(MCB), tawi la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, Bi. Leticia
Ndongole, (wapili kushoto), akimkabidhi zawadi ya IPAD, Bw. Khamisi
Mmuka, kutoka wilayani Newala mkoani Mtwara, baada ya kuibuka mshindi
kwenye droo ya kampeni ya "weka akiba na ushinde" iliyochezeshwa na benki hiyo. Anayeshuhudia ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
BENKI
ya Mwalimu, (Mwalimu Commercial Bank plc), imewakabidhi zawadi washindi watatu
wa kampeni ya “weka akiba na ushinde’ ambapo mteja wa benki hiyo kutoka
wilayani Newala, Bw.Khamisi Mmuka, alijinyakulia zawadi ya IPAD.
Katika
hafla hiyo ya kukabidhi zawadi iliyofanyika Agosti 7, 2017 kwenye
tawi la Samora la benki hiyo, washindi wengine ni Bi.Flora Mbaule na Bi.Macrina
Yoram Kyando wote kutoka Temeke jijini Dar es Salaam ambao walijnyakulia vocha
za manunuzi.
Akizungumza
kweney hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Meneja Masoko wa MCB, Bi. Rahma Ngassa
alisema, kampeni hiyo ilianza Mei 18, 2017 ambapo mteja mwenye akaunti kila
anapoweka akiba ya fedha kiasi cha shilingi elfu hamsini (50,000) kwenyeakaunti
yake, aliingia moja kwa moja kwenye droo hiyo. “Na sio mteja wetu tu hata
mwananchi aliyefungua akaunti na kuweka kiasi kama hicho cha fedha naye pia
alipata fursa ya kushiriki.” Alifafanua Bi. Rahma.
Naye
Meneja wa tawi la Samora wa benki hiyo, Bi.Leticia Mmuka, alisema ingawa
kampeni hiyo imemalizika lakini amewahimiza wananchi kufungua akaunti kwenye
benki hiyo na wale wenye akaunti waendelee kuweka fedha zao kwani benki inatoa
huduma bora na zenye kuvutia wateja.
Alisema
huduma huizo ni pamoja na kutoa gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni
sukuhisho la kifedha kwa walimu, watumishi wa serikali, wafanyabiashara,
wakulima na wananchi kwa ujumla.
“Huduma
za kibenki zitolewazo na MCB ni pamoja na mikopo yenye riba nafuu, huduma ya
ATM iliyounganishwa na mtandao mpana wa UMOJA SWITCH uliosambaa nchi nzima.”
Alifafanua zaidi.
Aidha
kwa upande wao washindi wa zawadi hizo walisema, wamefurahishwa na jinsi benki
inavyowashirikisha wananchi na wateja kwenye kampuni kama hiyo na kuwataka
wananhi kufungua akaunti na benki hiyo ambapo huenda nao wakapata zawadi kubwa
zaidi ya walizopata wao.
“Nimefurahi
sana kushinda zawadi hii, kwani mimi ni mteja wa MCB kutoka mbali kidogo, hko
Neawala mkoani Mtwara, laini nimeibuka mshindi, nah ii inaonyesha hapakuwepo na
upendeleo wowote, nawashukuru sana MCB kwa zawadi hii.” Alisema mshindi wa IPD
Bw. Khamisi Mmuka.
Meneja Masoko wa MCB, Bi. Rahma Ngassa, akizungumza na waandishi wa habari baada ya zoezi la kutoa zawadi.
Mshindi wa vocha ya manunuzi, Bi.
Macrina Yoram Kyando, (kushoto), kutoka wilayani Temeke jijini Dar es
Salaam, akielezea furaha yake baada ya kuibuka mshindi.
Mshindi wa vocha ya manunuzi, Bi. Flora Mbaule,
(kushoto), kutoka wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, akielezea furaha
yake baada ya kuibuka mshindi.
Afisa wa Huduma kwa wateja wa MCB, Bi.Martha Gambosi, (kushoto), akimkabidhi vocha ya manunuzi mshindi wa kampeni ya "weka akiba na ushinde" Bi. Flora Mbaule kutoka wilayani Temeke.
Meneja wa tawi la Samora wa MCB, Bi.
Leticia Ndongole, (Kushoto), akimpongeza Bi. Flora Mbaule kwa ushindi
wake uliompatia zawadi.
Kiongozi wa watumishi wa MCB tawi la
Samora, Bw.Ombeni Kaale, (wapili kulia), akimkabidhi zawadi ya vocha ya
manunuzi, Bi. Macrina Yoram Kyando, kitoka wilayani Temeke jijini Dar es
Salaam, baada ya kuwa miongoni mwa washindi wa droo ya "weka akiba na
ushinde" iliyochezesha na MCB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa benki
hiyo, Bi. Rahma Ngassa, (wakwanza kushoto) na Menja wa tawi la MCB,
Samora, Bi. Leticia Ndongole
SHARE
No comments:
Post a Comment