Mshindi wa Tuzo ya International
Confederation of Midwives (ICM), Loveluck Mwasha akiwasilisha mada
kwenye kongamano la kuadhimisha Siku ya Wakunga Duniani lililofanyika
Hospitali ya Taifa Muhimbili leo. Maadhimisho hayo yalianza wiki
iliyopita kwa kupima afya watu mbalimbali waliojitokeza katika hospitali
hiyo. Siku ya Wakunga Duniani huadhimishwa Mei 5, kila mwaka, lakini
TAMA tawi la Muhimbili iliamua kuadhimisha siku hii katika wiki ya
unyonyeshaji duniani.
Baadhi ya Wakunga na maofisa wengine wakifuatilia kongamano hilo leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika kongamano hilo wakunga wametakiwa kutoa huduma bora.
SHARE
No comments:
Post a Comment