Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw.
Francis Assenga (wapili kulia) akimkabidhi fulana na kofia Mkuu wa Mkoa wa
Lindi, Godfrey Zambi (kushoto) zitakazotumika wakati wa kilele wa Maadhimisho
ya Siku na Nane Nane kitaifa mjini Lindi.
Na Mwandishi wetu
Katika kudhirisha
umuhimu wa Siku ya Nane Nane Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)
imeunga mkono kwa kutoa fulana na kofia zitakazovaliwa katika siku ya kilele
cha maadhimisho hayo.
Akizungumza wakati wa
makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Wageni Maalumu
uliopo katika Viwanja vya Ngongo mjini Lindi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw.
Godfrey Zambi alisema kuwa TADB imeonesha mfano kwa taasisi nyingine nchi kwa
kutambua umuhimu wa Nane Nane inayofanyika kitaifa mkoani humo.
“Tunaishukuru sana TADB
kwa mchango huu ambao kwa hakika utang’arisha maadhimisho yetu,” alisema.
Bw. Zambi aliongeza kuwa
mchango huo unachagiza kauli mbiu ya Maonesho hayo isemayo “Zalisha kwa tija mazao
ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati”.
Kwa upande wake, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa Benki ya Kilimo
imeunga mkono Maonesho hayo ya Nane Nane kwa kutambua umuhimu wa kilimo na
kutimiza malengo ya Benki hiyo katika kusaidia kilimo nchini.
“Mchango huu unasadifu
malengo ya kuanzishwa kwa TADB ambayo yanajumuisha Kusaidia upatikanaji wa
utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania; na
Kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha
kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na
kupunguza umaskini,” alisema Bw. Assenga.
Maadhimisho
ya maenesho hayo yatafikia kilele siku ya tarehe 08 ambapo Mgeni rasmi wa
anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.
Meneja
wa Mikopo wa TADB, Samuel Mshote (kulia) akiwaonesha wanahabari ujumbe wa
Maadhimisho ya Nane Nane kwa mwaka 2017 kabla ya makabidhiano rasmi ya fulana
na kofia kwa Kamati ya Maandalizi ya Nane Nane kitaifa mjini Lindi.
SHARE
No comments:
Post a Comment