Korea Kaskazini
imeapa kulipiza kisasi na kuhakikisha kuwa Marekani imelipia gharama,
kwa kubuni vikwazo vya Umoja wa Mataiafa kufuatia na mpango wake wa
silaha za nuklia.
Vikwazo hivyo vilivyoungwa mkono kwa kura nyingi na Umoja wa
Mataifa siku ya Jumamosi "ni ukiukaji ya uhuru wa nchi," shirika la
serikali la habari la Korea Kaskazini KCNA lilisema.Kwa upande mwingine Korea Kusini inasema kuwa Korea Kaskazini imekataa ombi la kutaka wafanye mazungumzo.
Vikwazo hivyo vililenga kuzuia mauzo ya bidhaa za Korea Kaskazini kwa theluthi moja.
Vikwazo hivyo vya Umoja wa Mataifa vilifuatia majaribio ya mara kwa mara ya makombora yanayofanywa na Marekani, hali ambayo imeuzua wasi wasi kwenye rasi Korea.
Leo Jumatatu Korea Kaskazini ilisema kuwa itaendelea na mpango wake wenye utata wa kuunda zana za nuklia.
Kupitia kituo cha habari cha serikali cha KCNA, Korea Kaskazini ilisema kuwa haiwezi kuachana na mpango wake wakati inakabiliwa na vitisho kutoka Marekani.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment