Waendesha mashtaka
nchini Korea Kusini wanataka naibu mwenyekiti wa kampuni ya Samsung Lee
Jae-yong kupewa kifungo cha miaka 12 jela.
Inaripotiwa kuwa alitoa pesa nyingi ili apate uungwaji mkono wa serikali. Amekuwa gerezani tangu mwezi Februari kufuatia sakata hiyo lakini anakana kufanya lolote baya.
Wakati wa siku ya mwisho ya kusikilizwa kwa kesi yake, waendesha mashtaka walimtaja kuwa mtu aliyenufaika kutokana na uhalifu uliofanyika wakati wa sakati hiyo.
- Mbunifu wa Android azindua simu mpya
- Rais wa zamani wa Korea Kusini ashtakiwa
- Simu mpya ya iPhone isiyotumia headphone
- Simu zilichangia vifo vingi zaidi kwa kusababisha ajali Marekani
Waendesha mashtaka walidai kuwa ufisadi huo ulikuwa na lengo la kupata uungwaji mkono wa serikali kwa mabadiliko ndani ya kampuni ya Samsung.
Hukumu inatarajiwa kutolewa tarehe 27 mwezi huu wakati kuzuizi cha bwana Lee kitafikia mwisho.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment