Jimbo la Los
Angeles limeteuliwa rasmi kuandaa mashindano ya Olimpiki ya wakati wa
majira ya joto mwaka 2028 katika makubaliano yatakayoihakikishia Paris
kuandaa Olympiki ya mwaka 2024.
Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach amesema anakaribisha uamuzi huo wa Los Angeles kukubali kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa tarehe za mbele.
Kamati hiyo ya Olimpiki imesema itatoa mchango wake wenye thamani ya dola bilioni 0.8 kwa mji wa Los Angeles ili kufidia gharama zitakazoongezeka.
CHANZO; BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment