Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imetangaza majina manane ya wagombea
ambao yamepita katika mchujo wa awali kuwania nafasi mbalimbali katika
Kamati ya Uongozi (Management Committee) ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania
Bara.
Waliopitishwa ni kuwania uenyekiti
wa Management Committee ni Clement Sanga na Ahmed Yahya wakati Shan
Crysostoms ameiptishwa kuwania nafasi ya makamu mwenyekiti.
Kwa mujibu wa kamati hiyo,
Ramadhan Mahano na Hamisi Madaki wamepitishwa kuwania nafasi ya Ujumbe
wakitokea klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
James Bwire na Almas Kasongo
wamepitishwa kuwania Ujumbe wakitokea klabu za Ligi Daraja la Kwanza.
Brown Ernest hakupitishwa kwa sababu hakuthibitishwa na klabu yake.
Edga Chubura amepitishwa kuwania ujumbe akitokea klabu za Ligi Ligi Daraja la Pili.
Wagombea kwa mujibu wa kanuni
za uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu ni marais au wenyeviti wa klabu
husika. Wagombea wanatakiwa kuwa wenyeviti au Marais wa klabu husika.
Nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inagombewa na klabu za Ligi Kuu pekee.
Uchaguzi huo wa kamati hiyo
utafanyika Jumapili Oktoba 15, 2017 jijini Dar es Salaam na unaendeshwa
kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.
SHARE
No comments:
Post a Comment