Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Afrika Kusini
tayari kwa kuhudhuria mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika ( SADC) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. (PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
NA OMR,
PRETORIA
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili
nchini Afrika ya Kusini tayari kwa kuhudhuria Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na
Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC unaoaanza tarehe 19
na 20 ambapo leo tarehe 18 atahudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na
Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit).
Mheshimiwa
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Waziri wa Mawasiliano
wa Afrika Kusini Mhe. Ayanda Dlodlo.
akimuwakilisha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli.
Akizungumza
mara baada ya kuwasili kwa Makamu wa Rais, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augastine Mahiga amesema Mkutano
huo utapokea na kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa Mwenyekiti na
Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa
Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama; Hali ya Michango
mbalimbali ya Nchi Wanachama na Kupokea taarifa ya Mwenyekiti anayeondoka wa
SADC Organ.
Pia
Mkutano utapokea taarifa ya Katibu Mtendaji wa SADC; Kupitia hali ya kiuchumi
katika Kanda ya SADC; Kuwasilisha Kaulimbiu ya Mkutano wa SADC; Taarifa kuhusu
Mfuko wa Maendeleo wa SADC; Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa
Viwanda; Kuwezesha Chuo cha Elimu ya Sayansi na Teknolojia; Maombi ya Serikali
ya Comoro na Serikali ya Burundi kujiunga na SADC; Utekelezaji wa Mabadiliko ya
Kitaasisi ya Umoja wa Afrika na Mkutano wa Mshikamano kati ya SADC na Saharawi
ya Magharibi.
Dkt.
Mahiga amesema katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika
Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit) Tanzania itakabidhi nafasi ya
Uenyekiti kwa Mwenyekiti mpya.
Double
Troika inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania,
Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji. Katika mkutano huo Mfalme Mswati
III wa Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti. Ajenda kuu katika Mkutano huu ni
kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama
katika Kanda na hasa nchini DR Congo na Lesotho.
SHARE
No comments:
Post a Comment