Wateja
kushinda zawadi murua ikiwemo pikipiki na TV za kisasa kwa kununua simu
za Tecno S1 na Tecno R6 kutoka maduka ya Tigo nchi nzima.
Kampuni
inayoongoza kwa maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania imezidi
kuwaneemesha wateja wake baada ya kuzindua promosheni kabambe ambayo
inawapa wateja nafasi ya kushinda pikipiki na TV za kisasa kwa manunuzi
ya simu mpya aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka kwa maduka ya Tigo nchi
nzima.
Akizungumza
katika uzinduzi wa promosheni hiyo murua iliyofanyika katika makao
makuu ya Tigo jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde
Shisael alisema kuwa kupitia promosheni hii Tigo inahakikisha kuwa kila
mtu sasa ana nafasi ya kumiliki simu bora ya kisasa kwa bei nafuu. Ikiwa
ni muendelezo wa juhudi za Tigo kukuza mabadiliko ya dijitali nchini..
Pamoja
na hayo, kwa manunuzi ya simu aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka
maduka yote ya Tigo nchini, wateja wataingizwa kwenye droo itayowapa
nafasi ya kushinda mojawapo ya pikipiki 20 na televisheni 20 za kisasa
zinazoshindaniwa katika promosheni hii.
Shisael
aliongeza kuwa kila mteja atakaponunua simu aina ya Tecno S1 na Tecno
R6 kutoka maduka ya Tigo, wafanyakazi wa Tigo watanakili namba maalum ya
utambulisho ya simu (IMEI) pamoja na jina na namba ya simu ya mteja
husika aliyenunua simu. Namba hizi zitaingizwa katika droo za kila wiki
ambapo kila wiki, wateja watapata nafasi ya kujishindia mojawapo ya
pikipiki mbili na TV mbili zitakazoshindaniwa katika droo za wiki.
‘Promosheni
hii ya Tecno S1 na Tecno R6 inahusu tu wale wateja watakaonunua simu za
aina hii kutoka kwa maduka yetu ya Tigo nchini kote. Simu ya Tecno S1
ni ya mfumo wa 3G na itapatikana kwa bei ya shilingi 99,000/- tu. Simu
ya Tecno R6 ni ya mfumo wa 4G na itapatikana kwa bei ya shilingi
195,000/- tu. Simu zote mbili ni za kisasa na zina uwezo wa kutumia
mfumo wa data, kwa hiyo wateja wataweza kutumia huduma bora za data za
3G na 4G kutoka Tigo, hii ikiwa inalingana na aina ya simu
watakayonunua’ alifafanua.
SHARE
No comments:
Post a Comment