Marekani na Uingereza wajitolea kusaidia uchunguzi wa kuuliwa Chris Msando
Marekani na
Uingereza wamejitolea kusaidia katika uchunguzi wa mauaji ya kutatanisha
ya kaimu mkurugenzi wa masuala teknolojia wa tume ya uchaguzi na mipaka
nchini Kenya IEBC, kabla ya kufanyijka kwa uchaguzi mkuu.
Chris Msando alikuwa msimamizi wa mifumo ya kompiuta kwenye uchaguzi ambao utaandaliwa Jumanne, mifumo ambayo ingezuia wizi wa kura.
Mwili wa Bwana Msando ulipatikana kwenye chumba kimoja cha kuhifadhia maiti jijini Nairobi jana Jumatatu.
- Meneja wa tume ya uchaguzi apatikana amefariki Kenya
- Meneja wa teknolojia wa tume ya uchaguzi Kenya atoweka
- Uchaguzi Kenya 2017: Darubini kupitia vijana watatu
Polisi wanasema kuwa mwili Msando pamoja na wa mwanamke ambaye hakutambuliwa, ilipatikana eneo la Kikuyu lililo viungani mwa mji wa Nairobi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City Mortuary.
Mawasiliano ya mwisho kutoka mwa Musando aliyafanya siku ya Jumamosi mwendo wa saa tisa alifajiri kupitia ujumbe wa SMS kwa mmoja wa wafanyakazi wenzake.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment