Marekani imetangaza
vikwazo kwa kampuni kadha za Urusi na Uchina na watu ambao inawalaumu
kwa kusaidia mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini inapinga mazoezi ya pamoja kati ya Korea Kusini na Marekani
- Marekani na Korea Kusini wafanya mazoezi ya pamoja ya jeshi
- Marekani yaijibu Korea Kaskazini kwa mazoezi ya kijeshi
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tilleron, wakati huo huo ameipongeza Korea Kaskazini kwa kujizuia siku za hivi karibuni.
"Hatujashuhudia urushaji wa makombora na vitendo vya uchokozi kutoka Korea Kaskazini tangu azimio la baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa lianze kutekelezwa," alisema.
Wizara ya fedha itaendelea kuongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini kwa kuenga wale wanaosaidia kuendelea kwa mipango ya nyuklia na ya makombora ya masafa marefu.
Hatua hiyo inamaanisha kuwa watu nchini Marekani na kampuni za Marekani haziruhusiwi kufanya biashara na kampuni zinazosaidia programu za Korea Kaskazini.
China ilijibu mara moja kwa kutoa wito kwa Marekani ikitaka irekebishe makosa yake ya kuadhibu makampuni ya China.
CHANZO: BBC
SHARE









No comments:
Post a Comment