Kumekuwa na
ongezeko kwa idadi ya watoto wanaotuimiwa kama washambuliaji wa
kujitolea mhanga na wanamgambo wa Boko Haram, kaskazini mashariki mwa
Nigeria, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
55 kati yao walikuwa ni wasichana walio na umri chini ya miaka 15 na kwenye kisa kimoja, bomu lilifungwa kwa mtot ambaye alikuwa amebewa na msichana mdogo.
- Watoto wachanga watumiwa na Boko Haram
- Nigeria: Watoto watekeleza shambulio
- UN yaonya watoto kutumiwa na Boko Haram
Kulingana na Umoja wa Mataifa, watoto 127 wametumiwa kama walipuaji kaskazini mashariki mwa Nigeria tangu mwaka 2014.
Wanamgambo wa Boko Haram mara kwa mara wamewatumia watoto, na wamewateka mamia ya wasichana wa shule na kuwalazimisha watoto wavulana kujiunga na jeshi lao.
CHANZO: BBC
SHARE









No comments:
Post a Comment