Wema Sepetu alivyofika mahakamani jana.
KESI
inayomkabili staa wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, jana ilichukua sura mpya
baada ya mawakili wa pande mbili, ule wa utetezi na Jamhuri kuchuana
kuhusu mkojo wa msanii huyo uliochukuliwa na kupimwa na Ofisi ya Mkemia
Mkuu wa Serikali wakati wa upelelezi wa polisi kuhusiana na mwanadada
huyo kudaiwa kutumia madawa ya kulevya.
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama
ya Kisutu, Thomas Simba, shahidi wa kwanza wa upande wa Jamhuri
aliyefahamika kwa jina la Elias Mulima kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa
Serikali akisoma ripoti ya uchunguzi alisema mahakamani hapo kuwa, mkojo
wa Wema baada ya kupimwa ulikutwa na chembechembe za bangi.
Hata
hivyo, wakili wa utetezi, Peter Kibatala, alisema ripoti hiyo iliyosomwa
na Mulima ina upungufu mwingi wa kisheria. Baada ya kutokea malumbano
hayo Hakimu Mkazi Simba aliwaomba mawakili wa pande zote mbili kuridhia
apate muda wa kuipitia taarifa hiyo ya Ofisi ya Mkemia Mkuu ili
itakapoendelea aweze kuitolea ufafanuzi.
Awali, kesi hiyo iliahirishwa
kusikilizwa kwa muda mahakamani hapo kutokana na wakili wa Wema
kutokuwepo hivyo ikaanza kusikilizwa saa 6:30. Kesi hiyo iliahirishwa
hadi Agosti 4, mwaka huu.
Katika
kesi ya msingi, Wema anatuhumiwa kukutwa na msokoto mmoja wa bangi na
vipande viwili vidogo vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.
Mbali na
Wema washitakiwa wengine ni wafanyakazi wake wa ndani Angelina Msigwa
(21) na Matrida Abbas (16), ambapo wote wanashtakiwa kwa kosa moja la
kukutwa na kiasi hicho cha dawa za kulevya.
Msanii huyo na wenzake hao
wako nje kwa dhamana ya wadhamini wawili waliosaini Sh. 5,000,000 kila
mmoja. Inadaiwa kuwa Wema na wenzake walitenda kosa hilo Februari 4,
mwaka huu, nyumbani kwake Ununio, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment