Christopher Chege Msando enzi za uhai wake.
Mkurugenzi
wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC,
Christopher Chege Msando ambaye alitoweka siku ya Ijumaa usiku,
amepatikana akiwa amefariki.
Mawasiliano
ya mwisho kutoka mwa Musando aliyafanya siku ya Jumamosi majira ya saa 9
alfajiri kupitia ujumbe wa SMS kwa mmoja wa wafanyakazi wenzake.
“Hakuna shaka kwamba aliteswa na kuuawa,” mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati ameambia wanahabari.
Jeneza lenye mwili wa marehemu.
“Swali
pekee lililo katika akili zetu ni kuhusu nani limuua na ni kwa nini
aliuawa siku chache hivi kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika,” shirika la
habari la AFP limemnukuu Chebukati akisema.
Polisi
wanasema kuwa mwili wa afisa huyo pamoja na wa mwanamke ambaye
hakutambuliwa, ilipatikana eneo la Kikuyu, Kaunti ya Kiambu jijini
Nairobi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City
Mortuary.
SHARE
No comments:
Post a Comment