TRA

TRA

Tuesday, August 15, 2017

Msami amzungumzia Diamond

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Msanii wa Bongo Flava na Dancer maarufu, Msami ameeleza ulipoanzia utaratibu wa wasanii kujiita Simba jina ambalo Diamond Platnumz amekuwa akilitumia.
Muimbaji huyo ameeleza kuwa wakati wanaenda kushiriki mashindano ya kudansi yeye na Mose Iyobo walipenda kutumia jina hilo hasa pale wanapokutana na dancer wenye uwezo wa chini zaidi yao.
“I think hata jina la Simba lilianzia kwa mimi na Mose, mimi nilikuwa nakutana na Mose ananiita Simba, namuita yeye Simba that time Diamond alikuwa anacheza lakini sio sana,” 
“Diamond ni mtu ambaye alikuwa anakuja kwenye mashindano ya dance. Hata nikienda kufundisha kule Wasafi Mose ananiitaga Simba, Diamond naye akawa ananiita Simba na mimi nikawa namuita Simba mpaka baadae limekuwa kubwa lakini lilivyoleta stori nyingi huwezi kuibuka na kusema utaonekana kuna vitu unahitaji,” amesema Msami.
Msami kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘So Fine’ ambayo amemshirikisha Chemical.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger