TRA

TRA

Sunday, August 20, 2017

MTANZANIA DKT. STERGOMENA TAX ATEULIWA TENA KUSHIKA WADHIFA WA KATIBU MTENDAJI WA SADC

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Mkutano wa 37 wa wakuu wa Nchi za Jumuiya Kusini mwa Afrika SADC, umemteua tena Mtanzania Dkt. Stergomena Tax, (pichani), kuendelea kushika wadhifa wa Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo mwishoni mwa kikao hicho mjini Ptetoria, Afrika Kusini.
Dkt. Tax tayari ameapishwa kushika wadhifa huo ambapo Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, alikuwa mjongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo iliyosimamiwa na Mwenyekiti mpya wa SADC, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.

 Dkt. Tax, akila kiapo baada ya uteuzi huo.
 Mwenyekiti wa SADC, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Tax(wapili kulia).
 Makamu wa Rais, akiwa kwenye kikao hicho
 Makamu wa Rais na ujumbe wake


Makamau wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka saini moja ya makubaliano katika mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika wakati wa kuhitimishwa kwa mkutano huo mjini Pretoria. 

Mwenyekiti wa SADC, Rais Jacob Zuma akiendesha kikao cha 37 cha wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, wakati wa kilele cha mkutano huo, Agosti 20, 2017
 Dkt. Tax, akisaini kiapo hicho baada ya kuapishwa.
Dkt. Tax.(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger