IKITAMBULISHA
kikosi chake kipya ilkichosajili kwa ajili ya msimu huu wa ligi kuu
soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2017/2018 kwenye uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam, Simba ya Dar es Salaam ikionyesha kandanda safi na
lenye mpangilio, imewafunga mabingwa wa ligi kuu ya Rwanda, Rayon Sport
bao 1-0. Miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na timu hiyo na kuonyesha
kandanda safi na ya kiuvutia ni pamoja na kiungo wa zamani wa Yanga,
raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima na mshambuliaji wa xzamaniwa Simba,
Mganda Emmanuel Okwi.
Gyan
Okwi
Kocha Mkuu Omong
Jackson Mayanja
Manara
Msemaji
wa Simba Haji manara Akiwatambulisha Nahodha Msaidizi Mohamed Husein
kwa Mashabiki wa Simba Akiwa Sambamba na Nahodha wa Timu hiyo Mwanjali
Hadi
mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao hilo moja na kipindi cha pili
timu zote zilifanya mabadiliko Simba ikimuingiza kiungo wao hatari
Haruna Niyonzima kipenzi cha wana Yanga aliyehamia Msimbazi na alionesha
uhodari mwingi kwa kuuchezea Mpira kwa madaha.
Kama
Simbaa wangekuwa makini wangeweza kutoka na ushindi mnono kwani
mshambuliaji wao hatari John Bocco aliweza kukosa nafasi mbili za wazi
akiwa yeye na golikipa hadi mpira uanaisha Simba wameibuka na ushindi wa
bao 1-0 na kusherekea vizuri siku yao ya Simba Day ambayo imetimiza
miaka tisa tangu kuanzzishwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment