
Wachezaji wanne wa Yanga, Amissi Tambwe, Geofrey Mwashiuya, Obrey Chirwa na kipa Beno Kakolanya wameanza mazoezi.
Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amesema wachezaji hao wameanza mazoezi na wataanza kuonekana katika mechi zijazo.
“Hali zao zinaendelea vizuri na wataanza kurejea kuitumikia timu katika mechi zijazo,” alisema.
“Kuhusiana na suala la Buswita, hili linashughulikiwa na baada ya muda litapatiwa ufumbuzi,” aliongeza.
Buswita amefungiwa
kucheza Ligi Kuu mwaka mmoja baada ya kubainika amesaini timu mbili za
Simba na Yanga hata kumeibuka na ukakasi kwa wadau wapenda soka kutokana
na kifungo hicho kuwa ni cha kishabiki
SHARE
No comments:
Post a Comment