TRA

TRA

Saturday, August 5, 2017

RAIS MAGUFULI NA RAIS MUSEVENI WA UGANDA WAWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishikana mkono na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni baada ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga, katika sherehe iliyofanyika viwanja vya Chongoleani, Mkoani Tanga leo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni wakiwasili katika viwanja vya Chongoleani, Mkoani Tanga tayari kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni wakifurahi jambo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakiwa katika viwanja vya Chongoleani, Mkoani Tanga tayari kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (wa tatu kushoto), Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) pamoja na viongozi wengine wakiwa wamesimama wakati wimbo wa taifa ukiimbwa.
Wananchi wakishangilia wakati Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni wakiwasili katika viwanja vya Chongoleani, Mkoani Tanga tayari kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger