Afisa
Muuguzi Mwandamizi, Gudila Mambacho (kushoto) wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) akichukua vipimo vya presha toka kwa mmoja wa wananchi
(kulia) waliojitokeza kupata huduma za afya bure zinazotolewa na Chama
cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini
ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.Mmoja
wa maofisa kutoka Benki ya NMB (kushoto) akimuhudumia mwananchi
aliyejitokeza kupata huduma za kibenki kwenye kongamano la Chama cha
Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo
mbali na huduma hizo za kibenki toka NMB, wananchi walipata huduma
mbalimbali za afya bure, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya siku
ya wakunga duniani.Muuguzi
mwandamizi na afisa lishe kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dotto
Msabila Kafulie (kushoto) akimuhudumia mmoja wa wananchi aliyejitokeza
kupata huduma za afya bure zinazotolewa na Chama cha Wakunga Tanzania
(TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya udhamini mkuu wa
Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.Kutoka
kulia ni Maofisa Wauguzi na wataalam wa Kisukari Swaumu Gulumo na Sarah
Mwakilima wakimuhudumia mmoja wa wananchi (kushoto) waliojitokeza
kupima magonjwa mbalimbali bure katika kongamano la Chama cha Wakunga
Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni
maadhimisho ya siku ya wakunga duniani.Mmoja
wa maofisa kutoka Benki ya NMB (kushoto) akimuhudumia mwananchi
aliyejitokeza kupata huduma za kibenki kwenye kongamano la Chama cha
Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo
mbali na huduma hizo za kibenki toka NMB, wananchi walipata huduma
mbalimbali za afya bure, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya siku
ya wakunga duniani.Mmoja
wa maofisa kutoka Benki ya NMB (aliyeshika kipaza sauti) akizungumzia
huduma mbalimbali ya NMB kwa baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata
huduma anuai za afya bure zilizokuwa zikitolewa na Chama cha Wakunga
Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya udhamini
mkuu wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam, ikiwa ni shamra shamra za
maadhimisho ya siku ya wakunga duniani.Afisa
Muuguzi Mwandamizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Janeth Mwambona
(kushoto) akimuhudumia mmoja wa wananchi aliyejitokeza kupata huduma za
afya bure zinazotolewa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la
Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB
jijini Dar es Salaam.CHAMA cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali
ya Taifa Muhimbili chini ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB kimetoa huduma
za afya mbalimbali bure jijini Dar es Salaam, ikiwa ni shamra shamra za
maadhimisho ya siku ya wakunga duniani. Akizungumza jana na mwandishi wa habari hizi katika tukio hilo
linaloendelea Hospitali ya Taifa Muhimbili jirani na jengo la watoto,
Mwenyekiti Msaidizi wa Chama cha Wakunga Tanzania tawi la Hospitali ya
Taifa Muhimbili, Bi. Elizabeth Thawe aliwataka wananchi kujitokeza
katika eneo hilo ili kuweza kupata huduma hizo za afya bure. Alisema huduma wanazotoa bure siku nzima ya leo ni pamoja saratani ya
shingo ya kizazi, saratani ya matiti, elimu kuhusu lishe bora,
shinikizo la damu (BP), sukari mwilini na elimu ya unyonyeshaji watoto
kwa akinamama. “Kuelekea maadhimisho ya siku yetu, tumejitolea kupima afya bure kwa
wananchi wote watakaojitokeza katika eneo hili…huduma zinazotolewa bure
leo ni pamoja na saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti,
tunatoa elimu kuhusu lishe bora, tunapima shinikizo la damu (BP),
tunapima sukari mwilini na elimu ya unyonyeshaji,” alisema Bi. Elizabeth
Thawe. Aliongeza kuwa huduma hizo zinatolewa kwa wanachama wa Chama cha
Wakunga Tanzania (TAMA) tawi la Muhimbili kwa kushirikiana na wengine
kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Taasisi ya Mifupa
Muhimbili (MOI) pamoja na vyuo vyote vya afya vinavyozunguka Hospitali
ya Muhimbili. Alisema mbali na kutoa huduma hizo bure siku ya pili ya maadhimisho
(yaani Agosti 7, 2017) watafanya kongamano la kisayansi katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya siku
hiyo muhimu kwa wakunga. Aidha aliishukuru Benki ya NMB ambayo ni
wadhamini wa kuu wa maadhimisho hayo pamoja na makampuni mengine
yaliojitokeza kusaidia kufanikisha shughuli hizo. Mwandishi wa habari hizi alishuhudia misululu ya wananchi
waliojitokeza kupata huduma za afya bure eneo hilo na wengine kuvutiwa
na huduma za NMB zilizotolewa eneo hilo, kuwaunganisha wananchi na
huduma za kibenki. Maofisa
kutoka Benki ya NMB (kushoto) wakimfungulia akaunti mmoja wa wateja
(kulia) aliyejitokeza kupata huduma hizo katika kongamano la Chama cha
Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo
mbali na huduma hizo za kibenki toka NMB, wananchi walipata huduma
mbalimbali za afya bure, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya siku
ya wakunga duniani.Sehemu
ya wananchi wakiwa katika foleni kupata huduma za afya bure zilizokuwa
zinatolewa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya
Taifa Muhimbili leo.
No comments:
Post a Comment