
Mtafiti
na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Milemine East Refining Bw.
Salvatory Rwebangila akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati akielezea jitihada za Rais John Magufuli katika kutetea
rasilimali za taifa na kuokoa upotevu wa mapato, kushoto ni Afisa
uhusiano wa Taasisi hiyo Bi. Oliver Rwebangila na kushoto ni Afisa
Mipango wa taasisi hiyo Bw. Respikius Antony.

Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mtafiti na Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Milemine East Refining Bw. Salvatory Rwebangila (Katikati)
wakati akielezea jitihada za Rais John Magufuli katika kutetea
rasilimali za taifa na kuokoa upotevu wa mapato mapema hii jana jijini
Dar es Salaam.
Picha na eliphace marwa – Maelezo
…………………
Na Thobias Robert-MAELEZO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezidi
kupongezwa na wadau mbalimbali wa maendeleo juu ya hatua anazozichukua
katika kuliletea Taifa mabadiliko na maendeleo katika sekta mbalimbali.
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Milemine East Refining, Salvatory Rwebangila amesema
Mh.Rais amefanya mambo mengi ya kupongezwa tangu aingie madarakani baada
ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
“Siku
chache alizokaa madarakani ameweza kununua ndege kwa ajili ya Nchi hii
ambayo ilibakia ndoto baada ya kupoteza ndege zilizokuwepo awali, kwani
alipoingia madarakani shirika la ndege lilikuwa na ndege moja tu,
unaweza kujiuliza kwa miaka yote hiyo tulikuwa wapi? Kwa kipindi hiki
kifupi fedha zimepatikana wapi?” Alihoji Rwebangila.
Aidha,
Rwebangila alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imeondoa wafanyakazi
hewa zaidi ya elfu 19 pamoja na wafanyakazi wenye vyeti feki, waliokuwa
wananeemeka na rasilimali za nchi kwa njia zisizo halali. Aliongeza kuwa
rais ameokoa vijana wengi katika vita yake dhidi ya madawa ya kulevya
yaliyokuwa yanaangamiza nguvu kazi ya Taifa.
“Rasilimali
za madini zilikuwa zikisombwa kwa makontena na kuiacha nchi na zawadi
ya mashimo. Msimamo thabiti wa Dkt. Magufuli umemfanya kiongozi mkuu wa
kampnui ya Barrick kupanda ndege binafsi kuja kuangalia jinsi ya
kurudisha fedha zilizotokana na udanganyifu uliofanywa na Kampuni ya
ACACIA kwenye madini ya Tanzania,” alieleza Rwebangila.
Mbali
na mambo mengi ambayo Mh.rais amefanya, Rwebangila amempongeza kwa
kuanzisha ujenzi wa reli ya kisasa (Standard gauge) kutoka Dar es Salaam
hadi Morogoro, kuboresha huduma za kijamii pamoja na uamuzi wake
kuhamishia Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma.
“Ninampongeza
Mhe. Rais kwani utume wake umeinua watu ambapo sikudhani kwamba bado
tuna watu wa Mungu wenye uaminifu mkubwa wa kuyaona masuala ya hujuma
mbalimbali za rasilimali za nchi na watanzania wengi wamepata mbegu mpya
ya kulithamini taifa lao,” alieleza Rwebangila.
Kampuni
ya Milemine East Refining yenye makao yake Jijini hapa hujishughulisha
na utafiti juu ya malighafi za viwandani, madawa ya mimea, ubunifu wa
teknolojia na maji kuanzia miaka ya 1980.
SHARE
No comments:
Post a Comment