Siku tatu kabla ya
uchaguzi mkuu kuandaliwa nchini Kenya, muungano wa upinzani umeishutumua
serikali kwa kuvamia moja ya ofisi zake.
Lakini serikali imesisitiza kuwa hakuna uvamizi uliofanyika. Mgombea wa upinzani Raila Odinga amesema kuwa atakubali tu kushindwa ikiwa uchaguzi utakuwa wa haki.
Rais wa sasa Uhuru Kenyatta pia naye ameahidi kuheshimu matokeo ya uchaguzi huo wa siku ya Jumanne licha ya kila mmoja kusisitiza kuwa ataibuka mshindi.
Uchaguzi wa Kenya mara nyingi umekubwa na ghasia. Zaidi ya watu 1000 waliuawa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment