Mkurugenzi
Mtendaji wa SHUWASA,Injinia Silvester Mahole akizungumza katika warsha
ya kundi la wafanyabiashara wa hoteli na nyumba za kulala wageni mjini
Shinyanga Ijumaa Agosti 4,2017. Kushoto ni mwenyekiti wa warsha hiyo
Willium Shayo ambaye ni Mkurugenzi wa Evergreen Guest House na kulia ni
Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA, Deogratius Sulla-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
*******
Ijumaa Agosti 04,2017 Mamlaka ya Maji
Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) imekutana na kundi
la wafanyabiashara wa Hoteli na Nyumba za Kulala Wageni (Guest House and
Logde) mjini Shinyanga kwa lengo la kuwapa uelewa jinsi Mamlaka
inavyojiendesha sambamba na kupata maoni kutoka kwa wadau hao na kuweka
mikakati ya pamoja ya kuboresha huduma.
Akizungumza katika kikao
hicho,Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla alisema utoaji wa
huduma kwa wananchi una changamoto nyingi ambazo njia pekee ya kuzitatua
ni kushirikisha wadau wote.
“Mamlaka imekuwa ikitoa elimu kwa wadau
kuhusu namna mamlaka inavyojiendesha na kadri wadau wanavyoelewa kuhusu
haki na wajibu wao ndivyo wanavyoweza kushiriki kikamilifu kutatua
changamoto zinazojitokeza hivyo kuleta mshikamano zaidi baina ya mamlaka
na wadau wake”,alisema Mwenyekiti.
Wakichangia hoja katika warsha
hiyo,wafanyabiashara hao walisema kero kubwa waliyohitaji ifanyiwe kazi
haraka iwezekanavyo ni kukosekana kwa Mfumo wa Majitaka hali
inayosababisha watumie gharama kubwa kwa ajili ya huduma ya kuondoa
majitaka katika maeneo yao ya biashara.
Meneja wa Karena Hotel Richard Luhende
alisema kukosekana kwa mfumo wa majitaka kunawasababishia hasara
akitolea mfano wa hoteli hiyo kuita magari ya majitaka walau mara tatu
kwa wiki.
Naye Meneja wa Kisindi Lodge Agnes
Nyamwihula aliomba wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa uadilifu
ikiwa ni pamoja na kusoma mita zilizowekwa nje ya nyumba kwani baadhi
ya mita huwa hazisomwi matokeo yake Ankara ya maji inakuwa kubwa.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
SHUWASA,Injinia Silvester Mahole alisema mamlaka hiyo ipo katika mkakati
wa kuwa na mfumo wa majitaka mjini Shinyanga ingawa gharama za
kuendeshea mradi wa majitaka ni kubwa.
“Tayari tumeshapata eneo la kufanyia
mradi huu,tunafanya jitihada za kutafuta wafadhili,tatizo ni kwamba
wafadhili wengi wanaogopa kuwekeza katika mradi wa maji taka kutoka na
gharama zake kuwa kubwa zaidi ya mradi wa maji safi”,aliongeza Injinia
Mahole.
Katika hatua nyingine alitumia fursa
hiyo kuwahamisha wateja wa mamlaka hiyo kutumia njia za kisasa kulipia
Ankara zao kama vile kulipa kwa njia ya M-PESA,TIGO PESA au benki ya NMB
au Benki ya CRDB.
“Tunawashauri wateja wetu kubadilika
kulingana na maendeleo ya sayansi na teknolojia,tumeboresha huduma zetu
kwa kiwango cha juu sana,mbali na kulipa bill kwa njia ya simu,hivi sasa
unaweza kulipa kwa njia ya benki”,alieleza Injinia Mahole.
Injinia Mahole alizitaja baadhi ya
changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na gharama kubwa za
uendeshaji,uhaba wa nyenzo za kufanyia kazi,bomba za spea na presha
kubwa ya maji kutoka Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria hali inayosababisha
kupasuka kwa mabomba.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius
Sulla akifungua warsha ya kundi la wafanyabiashara wa Hoteli na Nyumba
za Kulala Wageni (Guest House and Logde) iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) leo Ijumaa
Agosti 4,2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Injinia
Silvester Mahole akizungumza katika warsha ya kundi la wafanyabiashara
wa hoteli na nyumba za kulala wageni mjini Shinyanga.
Injinia Mahole akizungumza katika warsha
hiyo.Kushoto ni mwenyekiti wa warsha hiyo William ShayoWillium Shayo
ambaye ni Mkurugenzi wa Evergreen Guest House,kulia ni Mwenyekiti wa
bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla.
Mwenyekiti wa warsha hiyo William
ShayoWillium Shayo ambaye ni Mkurugenzi wa Evergreen Guest House
akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Shayo akizungumza ukumbini.
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Injinia Silvester Mahole akielezea kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza kwa umakini mada iliyokuwa inaendelea.
Warsha inaendelea.
Ofisa Uhusiano wa SHUWASA, Nsianeli
Gelard akielezea kuhusu Haki na Wajibu wa mteja wa SHUWASA ambapo
aliwasisitiza wananchi kuwafichua watu wanaohujumu miundo mbinu ya
mamlaka hiyo na kuwaasa kulipa ankara kwa wakati na kuepuka kutumia
mafundi wa mitaani.
Sehemu ya mada ya Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard
Meneja Biashara wa SHUWASA, Reuben Mwandumbya akielezea kuhusu sheria inayohusu wizi wa maji.
Meneja wa Karena Hotel Richard Luhende akichangia hoja ukumbini.
Meneja Ufundi wa SHUWASA, Geofrey Hilly akizungumza ukumbini.
Meneja wa Kisindi Lodge Agnes Nyamwihula akichangia hoja katika warsha hiyo.
Meneja wa Katemi Hotel,Lameck Ntule akichangia hoja ukumbini.
Warsha inaendelea.
Ofisa Rasilimali watu na Utawala wa SHUWASA,Kambira Mtebe ambaye alikuwa MC katika warsha hiyo akikisisitiza jambo ukumbini.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment