Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus (kulia) akipokea cheti cha heshima toka
kwa Afisa Uhusiano wa Kampuni ya SportPesa Bi. Sabrina Msuya cha
kutambua mchango wa Idara ya Habari (MAELEZO) katika kufanikisha uratibu
wa vyombo vya habari wakati ujio wa timu ya Everton hapa nchini mapema
Julai Mwaka huu.
Cheti cha Heshima ilichopata Idara
ya Habari (MAELEZO) toka Kampuni ya SportPesa kwa kutambua mchango wa
Idara hiyo katika kufanikisha uratibu wa vyombo vya habari wakati wa
ujio wa timu ya Everton mapema Julai Mwaka huu.
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo
………………………..
Na.Paschal Dotto-MAELEZO.
Katika kutambua utendaji kazi wa
idara ya habari(MAELEZO) kampuni inayojishughulisha na mchezo wa
kubashiri ya Sportpesa leo imetoa Cheti cha Shukrani kwa Idara hiyo kwa
kushiriki vizuri katika ujio wa timu ya Everton nchini Julai mwaka huu.
Akizungumza katika makabidhiano
hayo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bw.Rodney Thadeus aliishukuru
kampuni hiyo kwa kutambua kazi nzuri ya Idara ya Habari (MAELEZO)
kuanzia kuwasili kwa timu hiyo kwa kuweka mazingira mazuri ya waandishi
wa habari.
Idara ya Habari ilifanya
maandalizi na uratibu wa vyombo vya habari kuanzia Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, uwanja wa taifa wakati timu ya Everton
inafanya mazoezi pamoja na siku mchezo wao dhidi ya Gor Mahia.
“Kwa mazingira yale ya wachezaji
wakubwa huwa wanahitaji sana usalama kwa hiyo mtu yeyote ambaye anataka
kwenda kuchukua habari lazima awe ametambuliwa na Serikali kupitia Idara
ya Habari (MAELEZO) na jukumu hilo tulilitekeleza kikamilifu
kuhakikisha kwamba hakuna mwandishi ambaye atazuiliwa kuingia uwanjani”,
alisema Bw.Rodney.
Bw. Rodney alisema kwamba
sportpesa wametambua kuwa kuna Idara ya Habari (MAELEZO) na kutambua
kwao inaonyesha jinsi gani Idara hii kuanzia kwa Mkurugenzi mkuu,
Wakurugenzi wasaidizi pamoja na maofisa wake wanafanya kazi
inayotambulika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Aidha Bw. Rodney alisema tuzo
hiyo itakuwa ni chachu ya kuendelea kufanya kazi kwa kasi zaidi katika
Idara hiyo ili kazi za Idara ziweze kufahamika zaidi, lakini kubwa zaidi
ni kuizungmzia Serikali na kazi zake katika Nyanja zote kuanzania
kwenye michezo na maeneo mengine ya uchumi, siasa pamoja na biashara.
Kwa uapande wake Afisa Uhusiano wa
kampuni hiyo Bi. Sabrina Msuya aliishukuru Idara ya Habari(MAELEZO) kwa
kazi nzuri wanayoifanya hususani kutoa ushirikiano katika kufanikisha
shughuli hiyo ya ujio wa timu ya Everton.
“Tunaishukuru Idara ya Habari
(MAELEZO) kwa kutupa ushirikiano wenu kufanikisha shughuli nzima ya
Everton kuanzia wanakuja, wakati wa mechi mpaka wanaondoka huu ni mwanzo
mzuri na tuanomba ushirikaiano wenu katika kuendeleza soka Tanzania “,
alisema Bi. Msuya.
Wakati wa ujio wa timu ya Everton
Idara ya Habari(MAELEZO) ikishirikiana na shirikisho la mpira wa miguu
Tanzania (TFF) ilihakikisha kila mwandishi anatekeleza majukumu yake ya
kihabari licha ya vibali vya waandishi kuisha jambo ambalo
liliwezekana.
SHARE
No comments:
Post a Comment