Staa wa filamu kutoka Marekani Nitara Carlynn Long maarufu kwa jina la Nia Long amewasili nchini wiki hii.

Nia
amewasili na muigizaji mwenzake anayefahamika kama Massai Dorsey. Wawili
hao wameletwa na shirika linalowashughulikia wakimbizi duniani UNHCR
kwa ajili ya kutoa elimu ya madhara ya ugonjwa wa Malaria katika kambi
ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo mkoani Geita.
Muigizaji
huyo ambaye pia ameonekana katika episode nane za tamthilia ya Empire,
kupitia mtandao wa Instagram ameonyesha kufurahia ziara hiyo kwa
kuandika, “Meet my new little friend! Today we distributed nets to her
family and I learned how to make cassava.”

SHARE
No comments:
Post a Comment