Msanii wa Filamu Bongo Jacqueline Wolper ameeleza sababu za yeye kuamua kuja na App.
Wolper atakuwa msanii wa pili kutoka katika tasnia ya filamu kufanya
hivyo baada ya Wema Sepetu. Wolper amesema moja ya sababu ni kuwa karibu
na mashabiki zake na kuwaepusha kupata taarifa za uongo kuhusu yeye.
“Yeah ni kweli nataka kuja na App yangu
na sababu kubwa ambayo imenifanya niwe na App ni kwa sababu mashabiki
wengi wanatamanigi kujua vitu vyetu kwa undani kwa sababu wanakutana na
facebook fake, wanakutana na mastori fake kwa hiyo ukiwa na App ni kitu
kikubwa zaidi kuwaweka mashabiki zako karibu,” alisema Wolper.
Pia ameongeza kuwa“Kuchart nao kuwajibu maswali yao na chochote ambacho wanakisikia wewe unawanyooshea maelezo”.
SHARE
No comments:
Post a Comment